HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 20, 2009

Alikufa Na Kuzikwa 2005... Akutwa Yupo Hai 2009 Mwanza!!



alipokuwa shule ya msingi

wakati wa mazishi yake huko Sweya Nyegezi, Kata ya Mkolani

akiwa katika Hospitali ya Bugando, wodi C-1 anakofanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wa akili

Na Jovin Mihambi, Mwanza

"SIKUAMINI macho yangu baada ya kugundua mwanangu ambaye nilimuuguza katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kuanzia Septemba 30 mwaka 2005 na baadaye kufariki dunia Oktoba 3, mwaka 2005, tukamzika baadaye ninakutana naye akiwa hai!"


Hayo ni maneno ya Bi. Stella Joseph ambaye ni mama mzazi wa binti anayedaiwa kufariki na baadaye kukutwa shambani miaka minne baadaye, Bi. Juliana Gembe (pichani).

Baada ya kifo chake, inadaiwa kuwa mwili wake ulizikwa katika makaburi ya Sweya-Nyegezi, Kata ya Mkolani, wilayani Nyamagana kwa heshima zote zikiwemo misa, sala na maombolezo kutoka kwa wakazi wa maeneo ya Sweya.

Aakizungumza na gazeti hili kwa uchungu, Bi. Joseph amesema kuwa binti yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria na alikuwa amelazwa katika wodi namba nane katika hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

Alsema baada ya binti yake kufariki dunia, uongozi wa hospitali ya Bugando ulitoa kibali cha mazishi chenye Nambari 0861800 cha Oktoba 3, 2005 na marehemu kuzikwa siku hiyo hiyo kwa kufuata utaratibu wote wa mazishi, na baba
paroko wa Parokia ya Mtakatifu Augustino, aliendesha ibada ya kumuombea marehemu.

Mama huyo anasema hazikuwepo hisia wala imani zozote za kishirikina kwa sababu yeye ni mcha Mungu na kuwa anajali sana maombi, hata kuliko dawa za hospitali au mitishamba kwa ajili ya kuponya magonjwa mwilini.

Anasema kuwa wakati akimuuguza mwanawe, mgonjwa huyo alikuwa akimwambia kuwa alikuwa anaona watu kadhaa wanafika kwa wingi kitandani mwake na kutaka kumchukua, na kuwa hata wakimchukua, atarudi tu na wala hawezi kuishi nao milele.

"Mama, naona watu wananisogelea kwa wingi kitandani hapa, eti wanataka kunichukua eti wanipeleke nikalime, ila mimi wakidhubutu kunipeleka, mie ni jeuri nitarudi tu
muda wowote," alisikika binti huyo akimweleza mama yake maneno ambayo yamenukuliwa na mama huyo.

Akisimulia jinsi binti huyo alivyopatikana akiwa hai, Mjumbe wa CCM, Shina Nambari 5 Kitongoji cha Buhima, Malimbe-Nyegezi, Bw. Sadik Ramadhani, amesema kuwa mnamo Oktober 15, mwaka huu majira ya saa 10.00 jioni, alishtukia umati wa watu ukifika nyumbani kwake na kumweleza kuwa kwenye ubalozi wake ametokea kiumbe wa ajabu mwenye jinsi ya kike ambaye ni wa kutatanisha.

Bw. Sadik alisema kuwa aliongozana na umati huo wa watu hadi mahali ambapo binti huyo alikuwa amekaa, huku akiwa akionekana kuchoka, kavalia matambala akiwa hawezi kuongea ila kwa ishala wakati alipokuwa akiulizwa kama anahitaji chakula.

Bw. Sadik amesema kuwa alimchukua binti huyo hadi nyumbani kwake huku akiandamana na watu hao na kumpikia ugali ambao alikuwa anaumeza bila kutafuna.

Amesema wakati akimchunguza zaidi, aligundua kuwa ulimi wake ulikuwa ndani na hauonekana huku akiwa na meno mawili moja likiwa juu na lingine chini. Pia mgogoni mwake kulikuwa na michirizi kama ya mtu ambaye alikuwa akichapwa fimbo.

Bw. Sadik anasema binti huyo kwa muda mrefu alikuwa amefumba macho hata mtu akijaribu kumfumbua
anayafumba tena, hali ambayo anaendelea nayo hata wakati huu akiwa katika wodi C-1 katika Hospitali ya Bugando akichunguzwa akili yake.

Bw. Sadiki amesema kuwa kadri watu walivyokuwa wakimininika kwenda kumwangalia, baadhi yao walimtambua kuwa ni binti ambaye alifariki mwaka 2005 na baadaye kuzikwa. Wengine ni wale ambao walikuwa wanasoma naye katika Shule ya Msingi, Nyamalango iliyoko Nyegezi, jijini Mwanza.

Amesema kuwa giza lilipoingia, ilibidi awatawanye watu wote waliokusanyika katika nyumba yake hadi siku iliyofuata wakati alipowasiliana na mtendaji wa Kata ya Mkolani ambaye alifika nyumbani kwake akiwa na polisi, wakamchukua hadi Bugando kwa uchunguzi zaidi.

Mama mzazi wa binti huyo anasema alipokuchunguza halama zote alizokuwa nazo binti yake wakati wa uhai wake, alithibitisha kuwa ni mtoto wake ambaye alifariki mwaka 2005.
endelea kwa kubofya hii link.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad