Jamani!Kwa nini tunakula sana kwa makusudi ili tuwe na vitambi
Mtu anaamka asubuhi, chai yake ni supu, mandazi matano,chapati na juice,kazini anapiga tena chai ya kababu,rosti maini,mchana ni wali au ugali, kwa nyama bakuli au nusu kuku,jioni kwenye baa, ni supu ya kuku,nyama choma mbuzi na kumalizia kwa kiti moto huku bia zikiendelea kama kawa,Nyumbani waifu huku akitaka mume anenepe(AJENGE HESHIMA KWA WAKWE NA WAMBEYA) anamlazimisha sinia la ubwabwa kwa nyama bakuli zima na mume lazima amalize kwa kuogopa soo( KUAMBIWA NANI KAKUPIKIA HUKO,UTANIELEZA).
Huyu bwana kashinda ofisini kwenye meza na kompyuta yake,kaenda kazini kwa gari,karudi kwa gari.Mbaya zaidi mazoezi anayasikia tu.Amekula chakula cha watu wawili na mwili wake umetumia nusu ya chakula cha mtu mmoja,kilichobaki kimehifadhiwa kama mafuta hasa kwenye maeneo ya tumbo na makalioni.Kumbuka huo ni mlo wa siku,jumlisha wiki,mwezi, mwaka,miaka ....!
NDIVYO TUNAVYOTAKA,MKE ANAFURAHI KAFANYA KAZI NZURI,KATENGENEZA KITAMBI,HAJUI NDIO ANAMTENGENEZEA MUME MAUTI,HALAFU JAMAA BAADA YA SIKU ANASHINDWA KUSHUGULIKA,SHIDA NDIO KWANZA INAANZA.
Je hakuna umuhimu wa wizara kuelimisha jamii kuhusu hili janga la VITAMBI VYA NYAMA CHOMA NA KITI MOTO na madhara yake lukuki kwa kizazi cha leo!Obesity,Overweight vimehusishwa navifo vingi vilivyotokana na Cardivascular disesases kama hypertension pamoja na Adult onset Diabetus.Kwa sasa ni silent killer,watu wanaanza kupoponyoka kwa kasi, Jamii na wahusika wako kimya.
Monday, September 14, 2009

Home
Unlabelled
Wapenda Vitambi Uwanja Wenu Kujielezea Juu Ya Mada Hii
Wapenda Vitambi Uwanja Wenu Kujielezea Juu Ya Mada Hii
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment