HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 1, 2009

Speech Zingine!!!

Jamaa mmoja ambaye ni mkurugenzi wa kampuni moja kubwa ya mawasiliano alikaribishwa kutoa speech katika tamasha moja la vijana lililokuwa limeandaliwa kuhusu kujiepusha na vitendo vyenye kuweza kusababisha maradhi ya kisasa Speech ya mkurugenzi huyu ilinukuliwa kama ifuatavyo:

Hali ni ngumu sana vijana kwa sababu kila mmoja anataka kuonja uzuri wa maisha ya kisasa. Mtandao wa ugonjwa huu ni mkubwa, mimi nashauri muwe makini . Jitahidini sana kukaa bila kupiga.. Ni muhimu simu zenu mzitunze sana na wala si kupiga piga kwani hiigharama yake ni kubwa. Kama shida ya kupiga itakuwa kubwa, basi hakikisha simu yako iko kwenye kipochi, na hivi vipochi vinapatikana kwa wingi na gharama yake si kubwa...

Hii inasaidia kupunguza uwezekano wa kupatamadhara yanayoweza kupatikana kutokana na mionzi iliyoko katika simu hizi sa kisasa. Ni mwiko kabisa kupiga tiGO kwa tiGO kwani hii ina hatari kubwa mno. Watu wengi simu zenu zina fanya kazi vizuri tu namna hamu angalau ya kubipu, lakini hii nayo ni hatari, kwani mwenzako akionyesha utashindwa kupokea ni rahisi sana kwako kuamua kupiga kabisa.

Msifikiri mkikaa bila kupiga muda mrefu, eti simu zenu zitamaliza chaji, hii si kweli. Hakikisha tu kwamba simcard iko katika hali nzuri, hii ndio ina kumbukumbu zote na ndio inaongoza mawasilianoyote.Simu ni simu tu, na madhumuni yake yanafanana.

Usidanganyike na simu kuwa eti ina camera au double screen hizo ni mbwembwe tu. Kuna simu nyingi sana feki siku hizi zinauzwa zimevishwa cover mpya, usidanganyike. Ukiona maisha bila kupiga hayawezekani, tafuta sehemu inayoaminika na uwe unapiga hapo tu, hii inasaidia sana kwani simu ukitumia peke yako inadumu zaidi kuliko ile yenye subscribers wengi.

BADILI TABIA KUPIGA SIMU OVYO SI SALAMA KWA AFYA YAKO.

Ahsanteni.

2 comments:

  1. YUKO SAWA,ILA TATIZO ALIONGEA KWA MAFUMBO HIVYO ASIYEKUWA NA UPEO WA KUONA NA KUSIKIA PIA KUFAFANUA HAWEZI KUELEWA KAMAANISHA NINI.ILA PIA ANAWAEPUSHA VIJANA KUTUMIA SIMU OVYO.MAANA AMBAYE HATO MUELEWA ANAMAANISHA NINI ATAMUELEWA KWA NJIA HIYO

    ReplyDelete
  2. Nimeipenda sana hiyo speech, imetulia, kwa aliye compose hii nampa hongera sana

    ReplyDelete

Post Bottom Ad