HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 10, 2009

Taji La Miss Lake Zone 2009 Lanyakuliwa Na Miriam Gerald

Pichani ni naibu waziri wa Africa mashariki Mh,Mohamed Aboud aliekuwa mgeni rasmi akimpongeza Vodacom miss Lake zone 2009 Miriam Gerald,onyesho hilo lilifanyika Yatch Club jijini Mwanza
Hatimae Miriam Gerald mrembo kutoka mkoa mwanza anyakua taji la vodacom miss lake zone,kulia kwake ni mrembo Mary Charles Alieshika nafasi ya pili, huku nafasi ya tatu ikirudi hukohuko mara kwa mrembo Sabina Budodi,namba nne ikishikiliwa na Glory Inosent mrembo kutoka Shinyanga,na namba tano alichukua mrembo Emakulata Alphonce kutoka Kagera.
Mgeni rasmi katika shughuli hii alikuwa Mheshimiwa Naibu Waziri wa ushirikiano Afrika mashariki,MOHAMED ABOUD.Ambae aliwakabidhi washindi zawadi zao,namba moja alipewa fedha taslim sh,laki sita,huku aliechukua nafasi ya pili akiondoka na kitita cha laki nne, na mshindi wa tatu sh, laki tatu, namba nne na tano walipewa sh laki moja na nusu.warembo wote walipewa zawadi zao ispokuwa mrembo namba tano Emakulata Alphonce kutoka kagera alipatwa na mshtuko na kupoteza faham aliposomwa na jaji mkuu kwamba ameshika namba tano,hivyo hakuweza kufika mbele kwani alikuwa amepelekwa hosipitali ya rufaa bugando,tunamshukuru mungu kwani kwa sasa anaendelea vizuri.

Kwa picha zaidi zama katika wanja la Da Flora kwa kubofya hiyo link
http://florasalon.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad