
Basi la Al-Hushum likisukumwa ili kuwekwa pembeni ya barabaya mara baada ya kubongana na basi la Scanlik katika eneo la Mahuga kilometa 80 kutoka Morogoro mjini,ajali hiyo ilitokea jana jioni mkoani Morogoro.

Basi la Scanlik likiwa limeanguka kiubavu mara baada ya kupata ajali ya kugongana na basi la Al-Hushum eneo la Maguha mkoani Morogoro.

Mmoja wa Majeruhi katika ajali hiyo iliyohusisha basi la Scanlik na basi la Al- Hushum akipatiwa matibabu na mmoja wa madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya kupata ajali.Utafiti unaonyesha kuwa,zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania hupata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali za barabarani zinazoendelea kutokea kila siku kutokana na uzembe na uendeshaji mmbaya wa haya mabasi.sasa sijui Serikali inalichukulia vipi hili swala??.picha zote na Mtangazaji Blog
kuna mwimbo wa zamani unaimbwa[safari sio kifo mamayeye subiri nitarudi mamawatoto.........} lakini kwasasa BONGO kusafiri inabidi ufikiri mara tatu. RIP to all.
ReplyDeleteMie hadi naogopa kusafiri na mabasi nijapo Tanzania maana ni hatari sana.
ReplyDeleteHivi ni picha au macho yangu? Iwapo hospital kubwa mgonjwa kalazwa kwenye gorodo kusiko kitanda.. hizo hospitals ndogo wilayani ndio itakuwaje?
Asante kutuletea habari.
Mama M.
Dah!!
ReplyDeleteLabda swali sio "mpaka watu wangapi wafe?" bali tubadili na kuuliza "watu ni kina nani?"
Inauma saaana
Niliwahi kuandika (http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/01/tumechoshwa-na-salamu-za-rambirambi-na.html) na natumai wengi tukishachoshwa, tukaonesha kukerwa, kisha tukasema basi tutabadilishiwa aina hii ya uzembe uuao wengi.
Blessings