
safu nzima ya ushambuliaji ya bendi ya msondo ngoma (Baba ya muziki) ikiwa stejini kuwakilisha libeneke kwa wadau wao,leo pale kizota pab ndani ya viwanja vya maonyesho ya biashara za kimataifa vya Mwalimu J.K.Nyerere(Saba Saba)

mkaanga chips wa msondo ngoma akiwajibika ipasavyo huku mwimbaji wa bendi hiyo akisikiliza kwa makini chips zikikaangwa.

Romario Mng'ande akifanya vitu vyake

Faza Maalim Muhidin Gurumo akiwajibika kama kawa,leo pale kizota pab

Mzee Said Mabela akiwajibika pamoja na vijana wake Romario na mwenzake

"Duuh!! ansante sana mdogo wangu,maana tanu nianze kuimba hapa wewe ndio umekuwa wa kwanza kunizawadia"hivyo ndivyo anavyoonekana Romario kumwambia binti huyo alieenda kumtunza.Msondo ngoma wapo kila siku hapo katika viwanja vya sabasaba kuisapoti bia ya Safari laga mpaka maonyesho yatakapomalizika,kuanzia saa nane mchana mpaka saa moja jioni.
No comments:
Post a Comment