Haroun amekiri wazi kuwa amekuwa akipoteza nguvu nyingi kwenye kundi hilo ambalo amekuwa hafaidiki nalo,hivyo ameamua kubadili upepo na kuwa msanii wa kujitegemea atakae fanya kazi zake binafsi.
"Mbali ya sababu hizo kadhaa pia washabiki wangu wamekuwa wakiziulizia kazi zangu binafsi hawazipati,hivyo kwa sasa nazielekeza nguvu zangu kwenye kazi zangu pamoja na project nyingine ambazo naziandaa wa ujio mwingine mpya",amesema Inspekta ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kiitwacho tamu ya ndoa,wimbo unaodaiwa kuwa ni jibu la msanii mwingine aitwaye Mwana FA aliyeibuka na songi lake la Bado nipo nipo unaoonekana kuzua gumzo kwa washabiki wa muziki huo wa kizazi kipya.
Haroun anabainisha wazi kuwa yeye hana kinyongo wala bifu na mtu yeyote yule ama kundi lolote lile,amijitoa kwa kwa ajiri ya tu ya kujipanga upya na kuendeleza shughuli zake za kimuziki,anasema na kuongeza kuwa kama ikitokea kazi ya kufanya na kundi basi atatoa ushirikiano wa kutosha bila malumbano yoyote.
sasa sijui huu ni Mwaka wa Majini?maana ule uliopita uliitwa wa Shetani sasa huu utaitwaje?
No comments:
Post a Comment