HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 18, 2008

Harambee Ya Kumchangia Ndugu Yetu Athuman Hamisi

WAKATI MIPANGO YA KUMPELEKA NJE YA NCHI MPIGANAJI ATHUMANI HAMISI (PICHANI) ALIYEJERUHIWA VIBAYA KWENYE AJALI YA GARI ILIYOTOKEA MWISHO WA WIKI ILIYOPITA HUKO KIBITI, MARAFIKI WA KARIBU WA MGONJWA WAMEAMUA KUFUNGUA MFUKO MAALUMU WA KUMCHANGIA ILI KUMSAIDIA YEYE NA FAMILIA YAKE KATIKA WAKATI HUU MGUMU. MFUKO HUO UNAITWA
'SAIDIA ATHUMANI HAMISI APONE'


MWENYEKITI WA MFUKO HUO NI DADA ASHA BARAKA WA TWANGA PEPETA AKISAIDIANA NA KAKA ERIC SHIGONGO BOSI WA GLOBAL PUBLISHERS PAMOJA NA BALOZI WA ZAIN AMBAO TAYARI KILA MMOJA WAO AMETOA SHILINGI LAKI 3 KWA AJILI HIYO.
HALI YA MGONJWA BADO TETE NA JUHUDI KUBWA ZINAFANYWA NA MADAKTARI WA MUHIMBILI KITENGO CHA MOI KUMTIBU. KINACHOSUBIRIWA NI BARAKA ZA MADAKTARI HAO ILI ATHUMAN HAMISI ASAFIRISHWE HARAKA KWA MATIBABU NJE YA NCHI.
TAYARI KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI YA VODACOM IMEELEZA NIA YAKE YA KUSAIDIA KWA HALI NA MALI KUFANIKISHA MATIBABU YA ATHUMANI HAMISI POPOTE DUNIANI


MICHANGO YA KUTUNISHA MFUKO HUO WA SAIDIA ATHUMANI APONE UNASIMAMIWA NA DA' ASHA BARAKA NA ANAYEPENDA KUCHANGA ATUME KUPITIA AKAUNTI


ASHA R. BARAKA
A/C NO. 01J 2018672700
CRDB BANK
HOLLAND HOUSE BRANCH
DAR ES SALAAM
KWA MAELEZO ZAIDI PIGA SIMU NAMBA
+255 713 606 564

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad