Washiriki wa kumtafuta Balozi wa REDD’S 2008 waelekea Mwanza:
Warembo kutembelea kaburi la Nyerere Butiama:
Waahidi kusaidia zaidi wenye shidaDar es Salaam,
Julai 12, 2008
Washiriki wa shindano la kumtafuta Miss Tanzania mwaka 2008 leo (Jumamosi) wameelekea Mwanza kwa ziara ya mafunzo ya siku 7 kwa ajili ya kumtafuta Balozi wa mitindo wa kinywaji cha REDD’s.
Hayo yalifahamika wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Beautiful Tanzanie Agency, Irene Kiwia alipoongea na vyombo vya habari huko Bagamoyo katika hoteli ya Paradise Resort ambako warembo wamepiga kambi ya wiki tatu.Safari hiyo ya washiriki wa Miss Tanzania inawapa nafasi warembo wote 28 kugombea kinyang’anyiro cha Balozi wa mitindo wa REDD’s.
Katika ziara yao ya Kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma mkoani Mara, warembo hao watatembelea kaburi la baba wa taifa, hayati Mwl Julius K Nyerere. Sambamba na hilo watapata fursa ya kuongea na wazee kijijini hapo na kushiriki chakula cha mchana pamoja na Mkuu wa mkoa wa Mara.Pamoja na mafunzo ya urembo, ziara hiyo itakuwa na bonanza, shughuli za kijamii, mazoezi, michezo na kujifurahisha.
Kiwia alieleza kwamba mashindano ya mwaka huu yameboreshwa ili kutoa fursa ya maandalizi mazuri ambayo yatamtoa mshindi wa kuwakilisha kinywaji cha REDD’s.Naye Victoria Martins ambaye anashikilia taji hilo amewashukuru TBL kupitia kinywaji chao cha REDD’s kwa kumpa fursa ya kuwa Balozi kwa kipindi cha mwaka mzima.
”Kuwa balozi wa REDD’s kumeniweka karibu sana na jamii, binafsi ninaguswa sana na matatizo yanayowakumba watoto yatima na kuwa kwangu Balozi wa REDD’s kumenipa furas ya kuwasaidia”, alisema.Mshiriki namba 3 Miss Tanzania mwaka huu Irene Salala (21kutoka Kanda ya kati amesema kwamba akipata nafasi ya kuchaguliwa kuwa balozi wa REDD’s atajishughulisha na wazee kwani anaona ni kundi lililosahauliwa katika jamii.Kwa upande wake Angela Lubala (18) ambaya ni mshiriki namba 26 kutoka Temeke amewapongeza REDD’s na waandaji wengine wa mashindano hayo kwa maandalizi yao mazuri ya kambi.Tuzo ya Balozi wa mitindo wa REDD’s ilianza kwa mara ya kwanza mwaka 2005, mwaka wa kwanza kwa REDD’s kudhamini Miss Tanzania na anayeshikilia taji hilo kwa sasa ni Victoria Martins ambaye alikuwa mshindi namba nne wa Vodacom Miss Tanzania 2007.Zawadi za atakayeibuka kidedea ni pesa taslimu Tsh 2,500,000/ na posho ya Tsh 250,000/ kwa kipindi kisichozidi miezi 12 au mpaka atakapoteuliwa balozi mwingine.
Mshindi wa tuzo ya Balozi wa mitindo wa REDD’s atatangazwa siku ya fainali za VODACOM Miss Tanzania 2008 hapo Agosti 2.
Kwa habari zaidi wasiliana na:George Kavishe,
Redd’s Brand Manager,
+255 767 266786,
george.kavishe@tz.sabmiller.com
Mabhe Matinyi,
Silver Bullet,
Media Relations,
+255 712 785695,
mabhe@ayr.co.tz
No comments:
Post a Comment