HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 29, 2008

Rais Kikwete Aomboleza Kifo Cha Chacha Wangwe

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA KWA RAIS KIKWETE
Mheshimiwa Spika,

Nimepokea taarifa ya kifo cha Mbunge wa Tarime,kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA)Mheshimiwa Chacha Zakayo Wangwe kwa masikitiko makubwa.
Kupitia kwako, napenda unifikishie rambirambi zangu za dhati kwa wabunge wa Bunge lako Tukufu kwa kumpoteza mbunge mwenzao katika kipindi hiki ambacho wako katika kutekeleza majukumu yao waliyotumwa na Watanzania,ya uwakilishi.
Kwa masikitiko makubwa napenda kutoa salamu zangu za pole kwa wana familia,ndugu, wananchi wa Jimbo la Tarime,wanachama wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA)na Watanzania wote.
Kifo huleta masikitiko na majonzi mengi katika familia na jamii, naungana nanyi ndugu zanguni katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na maombolezo,Mwenyezi Mungu awape imani na subira katika kipindi hiki kigumu na huku tukimuombea ndugu yetu, Chacha Wangwe mapumziko mema peponi.
Amina.
Wenu,

Jakaya Mrisho Kikwete
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
29 Julai, 2008

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad