HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 9, 2008

Kuuliza Si Ujinga

naombeni mnitoe ushamba mwenzenu,hivi wakati ndege inapotua hizi ndude huwaga zinafunguka,sasa mimi mwenzenu nimejitahidi kufikiria lakini hola na ndio nakaona ni bora niombe msaada toka kweni wadau.hivi hizi ndude zinazofungukaga kwenye haya mabaya ya ngege kazi yake huwaga ni nini??

4 comments:

  1. kaka hayo yakifunguka ni sababu ya kupigwa na upepo ili kuwe na resistance ya kwenda mbela na kusaidia brake

    ReplyDelete
  2. hmmm mimi ni injinia wa ndege by profeshno......
    hivo yakifunguka yanasaidia balance ili ndege itue na si kuanguka.na isipo jifunua hivyo wakati wa kutua ujue itacrash.
    ni hayo tu jr siku nyingine uwe unachunguza mwenyewe sio kuulizauliza tu.

    ReplyDelete
  3. Kwa kawaida ndege huwa ina break za aina mbili, break kwenye mambo ya machenics na break kwenye mambo ya mfumo wa bodi lake unaotegemea upepo na hii kwa kisayansi huitwa aerodynamics. Hii ndiyo hufanya ndege kupaa na kushuka. Sasa wakati wa kushuka ikishafika chini kabisa haya madude hujifunua kwa msaada wa nahodha ili kupunguza kasi ya ndege kwa kutumia upepo unaopita juu ua bawa na chini, na kwa ushirikiano wa break za kwenye matairi pia. Nadhani nimejaribu kukuelewesha.

    ReplyDelete
  4. Mabawa ya ndege yametengenezwa in such a way kwamba iisaidie ndege kuelea heawani ( mambawa yalivyotengenezwa upepo ukipipa chini ya ndege kunakuwa na High pressure na Juu kunakuwa na Low pressure)na hivyo kuifanya ndege ielee hewani...., wakati inapotaka kutua ni lazima kuondoa hiyo balance ndi maana mabawa yanafunguka na hivyo matairi yanakamata ardhi vizuri..., na wakati huuo huo nafunguka kwa chini vile vile kama additional brake ..., vile vile mabawa hutumika kama tanki la mafuta katika ndege.. nadhani nimekujibu

    ReplyDelete

Post Bottom Ad