HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 17, 2008

Hii Imekaaje Wadau?

Wadau wapendwa,
Hakika hili limenisikitisha sana na sina pa kulisemea zaidi ya hapa.
nilipoteza wallet yangu8 tarehe 21 ikiwa na id's zangu pamoja na ATM card yangu, sasa nikaenda bank niblock account yangu. Nikaambiwa haiwezekani hadi niende polisi nipewe lost report.
Hapo bank wakanipa form ya kunitambulisha huko polisi kama mteja wao. Nikaenda police pale Udsm mlimani , wakaandika maelezo yangu then nikaambiwa inabidi niende kituo cha magomeni au oysterbay nikalipie shilingi mia tano (500) kwa sababu wao hawana mhasibu pale, nipewe risiti niirudishe pale polisi ndio wanipe hiyo lost report ili nende bank kublock account yangu na kuanza process ya kupewa ATM mpya.
Kwa kuwa ilikuwa jioni definately nisingemkuta huyo mhasibu, nilivyoenda oysterbay nikaambiwa hawana risiti zimeisha niende magomeni, nikaenda magomeni nikaambiwa risiti zimeisha niende baada ya siku tatu au niende msimbazi, (kumbuka siku zinapita sija-block account yangu hapo), mchana huu nimeenda msimbazi, nimeambiwa risiti hakuna.
Sasa nikauliza inakuwaje kwenye ishu kama hii wananizungusha hivi na account yangu inaweza kuibiwa wanasema there is nothing they can do.
I am so mad hata sijui nfanyeje, tena bila aibu polisi huyo ananiambia rudi kule mlimani wabembeleze wape chochote wakuandikie lost report ndo hali ilivyo" can you imagine?
Yani nimesumbuliwa wiki mbili ili nilipie tu sh 500 nimetembea vituo vyote hivyo vya polisi na hakuna nilichokipata, sasa jamani kwa hali hii mtu anafanyaje? Je hii nchi haina kabisa utaratibu wa maana zaidi ya mlolongo mrefu usiokuwa na kichwa wala miguu ukitoa mianya ya rushwa?
Na sasa ni lazima kuwe na process ndefu namna hii kwenye huduma ambayo ni haki yangu?
Mdau Mwenye Usongo

1 comment:

  1. we mdau mwenye usongo pole sana.mi mwenyewe nilipoteza atm kadi yangu hivyo hivyo lakini nilipoenda kuandikisha polisi kituo kidogo wakanambia niende kituo kikuu buguruni kugonga muhuri na kuandikiwa risiti,na nilivyofika buguruni wakanambia ooh nirudi j3 kuandikiwa risiti nikamita chemba riafande limoja nikalitoa buku tu huwezi amini nikahudumiwa shida zangu zote.
    kwa hiyo we ulijizungusha bure.
    nakushauri tu we mpe mtu yeyote hela we mwambie tu ni ya usumbufu ili akuhudumie utashangaa na risiti na mihuri inapatikana.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad