HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 14, 2008

Habari Ndio Hiyo

MBUNGE wa Kyela,Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye Juni 12 aliugua ghafla akiwa bungeni mjini hapa, yu mzima na hajafa kama ambavyo leo kutwa nzima habari zilienezwa katika miji ya Dodoma na Dar es Salaam,Ofisi ya Bunge imeeleza. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari kwa Umma wa Bunge, Jossey Mwakasyuka,Dk. Mwakyembe hajafariki dunia na kwamba habari hizo ni uzushi kwani jana mchana alizungumza na Spika Samuel Sitta,na leo atasafiri kwenda Dar es Salaam.

Aidha,Mwakasyuka alisema kwamba Katibu wa Bunge amethibitisha kuwa Mwenyekiti huyo wa Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza mkataba wa Richmond,yu mzima. Katibu wa Bunge amesema uzushi huo wa kifo umelishtua Bunge.Dk. Mwakyembe aliugua ghaflaakiwa kwenye kikao cha Bunge mjini hapa na alikimbizwa katika Zanahati ya Bunge,ambako alipata huduma ya kwanza.
Tangu alipoongoza Kamati Teule ya Bunge, Dk. Mwakyembe amejipatia umaarufu mkubwa hasa kutokana na matokeo ya kamati hiyo ambayo yaliwalazimisha mawaziri watatu kujiuzulu, akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa,kwa sababu ya kuwajibika kutokana na kashfa hiyo.Wengine waliojiuzulu ni mawaziri wa Nishati na Madini,Nazir Karamagi na yule wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha.

1 comment:

Post Bottom Ad