
Amanda Ole Sululu - mrembo wa Tanzania anayeiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Miss Universe 2008 nchini Vietnam, ameingia katika 20 bora kati ya warembo 80 waliokuwa nchini Vietnam.
Amanda ambaye alishinda taji la Miss Universe Tanzania tarehe 29 Mei 2008, alitayarishwa na wataalam mbalimbali hapa nchini chini ya usimamizi wa kampuni
ya Compass Communications.

Mavazi ya mwanadada huyu ikiwemo vazi la jioni,(evening gown) yameandaliwa na Maua Mazuri. Vazi la Taifa(national costume) limebuniwa na mbunifu mashuhuri toka visiwani Zanzibar, Farouque Abdela.
Vazi hili la taifa limebeba ujumbe mzito wa kutunza mazingira kwani gauni limetayarishwa kwa kutumia mifuko ya plastiki maarufu kama mifuko ya rambo. Gauni na mrembo mwenyewe amenakshiwa na mapambo ya kimasai. Amanda Ole Sulul ambaye ni Maasai ameweka nia ya kutangaza vyema utamaduni wake wa kimasai na utamaduni wa kitanzania kwa kuvaa magauni na nakshi za kiasili.
Amanda pia atavaa vazi la jioni lililotayarishwa na mbunifu chipukizi Ally Rhemtullah (siyo picha alilovaa katika picha hii).
Amanda pia amepeleka zawadi maalum la kitaifa la begi lililotengenezwa na mkeka na ngozi iliyobuniwa na Farouque Abdela.

Amanda pia amepeleka zawadi maalum la kitaifa la begi lililotengenezwa na mkeka na ngozi iliyobuniwa na Farouque Abdela.

Kama sehemu ya maandalizi yake na zawadi yake, mrembo Amanda amepewa vipodozi bora vyenye hadhi ya kimataifa na kampuni ya Shear Illusions. Vilevile kupitia mama Hasina Kassongo na kituo chake cha mazoezi cha Fitness centre, walihakikisha kuwa mwili wake mrembo uko fiti katika kuujenga na kuonekana ipasavyo.
Kwa upande wa saikolojia, Amanda aliandaliwa na mtaalam Mike Lerch. Mrembo wa mwaka jana Flaviana Matata alimpa mrithi wake Amanda mazoezi na mbinu ya kutawala jukwaa.Akiongea kwa njia ya simu, Amanda ameomba watanzania waendelee kumwombea ili aweze kupeperusha bendera ya Tanzania vyema na kuiletea sifa nchi yetu.imeandikwa na Mkuu Issa Michuzi
No comments:
Post a Comment