HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 24, 2008

Visura Wetu Hawa

Visura 5 wanajianda kwa ajili ya fainali ya kumpata kisura wa Tanzania (Face of Tanzania) itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 26 mwezi wa 4, Movenpick Hotel wakisindikizwa na Tatiana Derao ambapo atakuwa mmoja wa majaji.
Kutakuwa na burudani ya bendi ya Kilimanjaro [wananjenje] na chakula cha usiku.
Shindano la kumpata kisura wa Tanzania lilianza na washiriki 16 ambao walichaguliwa kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania. Baada ya usaili wa mikoani, waliochaguliwa waliingia kambini tarehe 5 mwezi wa 3 jijini Dar-es-Salaam.
Hapo kambini walipewa mazoezi mbali mbali yanayohusika na mambo ya uanamitindo ikiwemo upigaji wa picha na kujifunza ku tembea stejini.Kila wiki majaji walikuwa wanachuja visura watatu na kisha kupigiwa kura na watazamaji wa kipindi na kubaki kisura mmoja.
Kura zinapigwa kwa njia ya SMS kwenda namba 15551 na kipindi kinarushwa na Shirika la utangazaji Tanzania [TBC] kwa wiki mara mbili [Jumatano na Jumapili saa moja usiku].
Visura walichujwa kutoka 16 kufikia 5 bora ambao walisafiri kwenda Afrika ya Kusini kujifunza mambo mbali mbali ya uanamitindo pia na kukutana na wanamitindo wa kimataifa kwa muda wa wiki moja.
Sasa hivi visura wanajianda kwa ajili ya fainali itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 26 mwezi wa 4, Movenpick Hotel wakisindikizwa na Tatiana Derao ambapo atakuwa mmoja wa majaji. Kutakuwa na burudani ya bendi ya Kilimanjaro [wananjenje] na chakula cha usiku.
Ticketi zinauzwa kwa bei ya Tshs 100,000.00 pia zinauzwa kwa meza ya watu wanane kwa Tshs 700,000.00. Tcketi zinapatikana kwenye vituo vifuatavyo: Renzo Salon [Mikocheni], Novel Idea [Town], Steers [Town], Shear Illusions [Millenium Towers], Steers [Millenium Towers] and Engen Petrol Station [Mbezi Beach].
Wabunifu watakao onyesha nguo zao ni kama ifuatavyo: Ally Remtulla, Zamda George, Robbi Morro, Napelel Africa na Francissca Shirima.
Mshindi wa shidano la kisura atapata mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya O Model Africa ya Afrika ya Kusini wenye thamani ya dola za kimarekani 52,000.00 na ataanza mkataba rasmi mwisho wa mwezi wa 5 2008.Visura waliofanikiwa kuingia 5 bora ni kama ifuatavyo: Emmy Melau kutoka Arusha, Edna Makanzo kutoka Dar-es-Salaam, Neshino Laizer kutoka Karatu, Yvonne Ramomi kutoka Zanzibar and Irene Shirima kutoka Arusha.
Watazamaji wanahamasishwa kuwapigia kura mshiriki umpendae kwa kutuma neno ‘kura’ acha nafasi alafu jina kwenda namba 15551.
Shindano hili limeandaliwa na kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency na kudhaminiwa na makampuni ya Tanzania Broadcasting Corporation, Coca-Cola, Bang Magazine, Clouds FM, Regency Park Hotel, Air Tanzania, Renzo Salon, Redds Premium Cold, Highview hotel, New Habari Corporation na Legend Lodges.

2 comments:

  1. Ninawapa hongera sana kwasasa, madada zetu wamependeza wotee. pia ninakusalimu sana Michuzijr, pia kwako nipo.

    ReplyDelete
  2. kaka nashukuru sana kwa pongezi za hawa dada zetu,na salam zako kaka zimefika kama kawa

    ReplyDelete

Post Bottom Ad