HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 14, 2008

Fikiri Wangepewa Mtihani Huu Fred Na Edward!

Wachukuliwe kwa gari wote wawili. Washushwe Magomeni Mwembechai kisha waambiwe; tembeeni kwa miguu bila walinzi wala wapambe. Mkatishe Tandale, Manzese Uzuri na mwisho mtokee Sinza Kijiweni. Naamini Fred angefaulu kukatisha na labda kuna wawili watatu njiani wangemwuliza maendeleo ya mashamba yake ya Kibaigwa na ng'ombe wake kule Kibaha. Vinginevyo, pamoja na kashfa zake za mashamba ya Kibaigwa, Mkopo wa milioni hamsini Nssf na safari ya Marekani iliyogharimu shilingi milioni mia tano, bado Fred angekanyaga Sinza Kijiweni akipiga miruzi na mikono mfukoni. Lakini, kwa joto hili la sasa la Richmond na hasira za wananchi, nahofia Edward safari yake ingeishia Tandale. Labda wanakijiji wenzangu mna mtazamo mwingine.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad