HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 5, 2007

Mfadhili Toka Majuu

kuna msela wetu flani kanirushia hii,bila hiyana nami naiwakilisha kama kawa kwenu masela wangu

Ifuatayo ni sehemu ya hotuba ya Mfadhili (Mzungu) wa mradi wa maji safi huko katika kijiji cha Mkomazi, Mkoani Tanga.
Mfadhili huyu kutoka ubalozi wa nchi moja - Majuu amewahi kujifunza kiswahili kwa muda wa miezi mitatu hivyo kutohitaji kufuatana na mkalimani wa ubalozi.
Alikuwa na hayamachache:
Mzungu: Jambo wanakijiji wa Mkuma Wazi?
(akimaanisha Mkomazi)
Watu walibaki kumtumbulia macho na kujikausha wengine Wakicheka kichini chini. Mzungu akadhani amepatia sana lugha ya kiswahili, akazidi kujitutumua:
Leo mimi na uke yangu (mkewe!)tumekuja hapa Mkuma wazi kukagua
mitombo ya mboo zenu inayoendeshwa kwa nguvu ya pepo
( Mitambo ya mbao inayoendeshwa kwa nguvu ya upepo!)
na Visimi yenu inatoa maji(Visima jamani!).
Mitombo hii ni pesa kidogo na wake yenu haitakuwa na maumivu zaidi kubeba maji.
Watu wakaduwaa kabisa!
Mzungu akaropoka tena:
Mbona watu mko pumbu wazi? (Alikuwa ana maanisha bumbuwazi
lililowapata wanakijiji! Wanakiji wakaanza kuzoza chini chini
hatimaye sauti zikawa za juu wakimuuliza Mzungu kwa nini
amewatusi kiasi hicho.)Mzungu wa watu akazidi kubomoka kiswahili:
Mzungu:
Pepo kubwa inafanya mitombo kufanya kazi bila kulala na visimi yenu
kutoa maji salama na mama wamepata uja zito na watoto yenu wanakuwa salama!

Wanakijiji wazidi kuzoza.

Mzungu:Nasema sikiliza watu wote, Kima, Nyama zenu!!!
Hapa alikuwa akitaka kusema watu wote kaeni kimya, nyamazeni!
Mzungu wa watu baada ya kufanikiwa kuwanyamazisha wananchi
akaendelea kuwaambia kwamba ameridhishwa na hali ya usafi wa visima
ikilinganishwa na siku za nyuma.

Mzungu wetu akaendelea kusema:
Mzungu:
Mimi na uke yangu tumechota maji kutoka visimi yenu na kuyaweka kwenye chupi yetu!
Akimaanisha wamechota maji toka kwenye visima na kuyaweka kwenye chupa.
Akazidi kubonga:

Mzungu:
Sasa mimi na uke yangu tutatoa chupi yetu na tutakunya mbele yenu!
lahaula lakwata wanakijiji waanza kuondoka:
Alikuwa anamaanisha kwamba watayamimina maji na kuyanywa mbele yao
ili kuwathibitishia kwamba ni safi na Salama.
Lugha ya watu bwana...
hii kali ya mwaka yaani hapa nimechoka kabisaaaaaaaaaaaa...

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad