HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 12, 2026

NAIBU KATIBU MKUU CCM ZANZIBAR ARIDHISHWA NA UJENZI WA HOSPITALI YA NUNGWI

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Ndg. Abdi Mahmoud Abdi, ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa Hospitali ya Nungwi, Mkoa wa Kaskazini ‘A’, akisema mradi huo utasaidia kutatua changamoto mbalimbali za huduma za afya kwa wananchi wa jimbo hilo.

Ndg. Abdi amesema ujenzi wa hospitali hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, yenye lengo la kuboresha huduma za afya na kuzisogeza karibu zaidi na wananchi.

Aidha, amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na viongozi wao kuanzia ngazi ya jimbo hadi taifa, katika kuhakikisha huduma za kijamii, hususan afya, zinaendelea kuboreshwa na kusogezwa karibu na wananchi.

Kwa upande wake, mkandarasi wa mradi huo amesema ujenzi wa kituo hicho cha afya chenye ghorofa mbili umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Desemba mwaka huu.






 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad