HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 21, 2026

Messi Afunga Goli la 101, Inter Miami Ikitoa Sare 2-2 na San Diego

 


Lionel Messi na Inter Miami wamepoteza nafasi ya kupunguza pengo lao kileleni mwa Eastern Conference ya MLS baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya San Diego katika mchezo uliochezwa usiku wa Kuamiakia leo jijini Florida.

Matokeo hayo yameifanya Inter Miami kubaki nafasi ya tatu wakifungana pointi 46 na New England Revolution huku ikiwa imesalia na michezo minane ya msimu wa kawaida wa Msimamo wa Estern Conference, Huku msimamo huo ukiongozwa na Nashville FC mwenye pointi 57

San Diego walianza mchezo kwa kasi na kupata bao la kuongoza dakika ya 12 kupitia mshambuliaji wa Denmark, Anders Dreyer. Dreyer alipokea pasi nzuri kutoka kwa Jeppe Tverskov, kabla ya kumzidi kipa Dayne St. Clair kwa kumpiga mpira wa juu na kuifanya San Diego kuongoza 1-0.

Inter Miami waliongeza presha baada ya bao hilo na hatimaye wakasawazisha dakika ya 24 kupitia Messi. Nahodha huyo wa Argentina alipiga free-kick kali kutoka nje ya eneo la hatari, mpira ukapita katikati ya wachezaji wengi ndani ya boksi na kugonga ndani ya nguzo kabla ya kuingia wavuni. Bao hilo lilikuwa la 101 kwa Messi akiwa na Inter Miami.

Kwa haya na mengine mengi ya kimichezo, tembelea Jukwaa la Meridianbet kwa Taarifa, takwimu, uchambuzi na matokeo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni.

“Messi, Luis Suarez na Rodrigo De Paul walipata nafasi nzuri, lakini San Diego waliweza kuendelea kujilinda na kuzuia mashambulizi ya Miami.”

Inter Miami walifanikiwa kupata bao la pili dakika ya 74 baada ya De Paul kumpa pasi nzuri Luis Suarez pembeni mwa eneo la hatari, ambapo mshambuliaji huyo raia wa Uruguay alimalizia kwa nguvu na kuifanya Miami kuongoza 2-1.

Hata hivyo, San Diego hawakukata tamaa na dakika za mwisho walipata bao la kusawazisha kupitia Dreyer, aliyepokea tena pasi ya Tverskov na kufunga kwa utulivu na kufanya mchezo huo kumalizika 2-2.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad