
Leo Jumamosi, Agosti 22, 2026, ligi kuu ya Uhispania (LaLiga) inaingia wiki ya pili ya ushindani, ikiwa na mchezo mzito kati ya Espanyol na Real Madrid katika uwanja wa RCDE Stadium, mjini Cornellà de Llobregat, karibu na Barcelona. Mchezo huu utaanza saa 22:30 usiku.
Zaidi ya ushindani wa kawaida wa ligi, mchezo huu unabeba historia kubwa ni mwanzo rasmi wa uongozi wa pili wa Jose Mourinho kama kocha wa Real Madrid, miaka 13 tangu alipoondoka klabuni hapo.
Mourinho amerejea Real Madrid akiwa na mkataba wa miaka mitatu baada ya kuteuliwa na rais Florentino Pérez mwezi Juni mwaka huu, kufuatia msimu mgumu uliopita ambao Real Madrid walimaliza wakiwa nyuma sana ya washindani wao wakubwa Barcelona.
Wakati wa uongozi wake wa kwanza kati ya 2010 na 2013, Mourinho aliwahi kuwapatia Real Madrid ubingwa wa ligi, Kombe la Copa del Rey na Supercup ya Uhispania. Sasa anarejea na jukumu kubwa la kuwarudisha "Los Blancos" kileleni mwa soka la Uhispania, huku akiwa ameleta wafanyakazi wapya na kufanya manunuzi makubwa msimu huu wa joto ili kutimiza dhamira hiyo.
Espanyol, kwa upande wao, wanaingia mchezoni wakiwa na hamasa kubwa baada ya kuanza msimu vizuri kwa kuwafunga Levante mabao 3-0 wiki iliyopita, huku mshambuliaji Roberto Fernández akichangia mabao mawili na Tyrhys Dolan akiongeza la tatu.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Timu ya kocha Manolo González itategemea sana nguvu ya wachezaji wao wa kati, hasa Javi Puado na kikosi kizima kilichoonyesha umoja mkubwa msimu wa kwanza wa mchezo. Hata hivyo, Espanyol watakosa huduma za Kike GarcÃa na Javi Puado kutokana na majeraha, jambo litakalowapunguzia chaguo mbele ya bao.
Kwa Real Madrid, mchezo huu utakuwa mtihani wa kwanza rasmi wa Mourinho tangu kurejea, na kikosi chake bado kina baadhi ya changamoto za majeruhi Aurélien Tchouaméni, Endrick, Thiago Pitarch, Raúl Asencio na Ferland Mendy wote hawatapatikana kwa mchezo huu.
Licha ya hayo, Real Madrid bado wana silaha kubwa mbele wakiwa na Kylian Mbappé, aliyekuwa mfungaji bora wa Kombe la Dunia 2026 na anayeendelea kuwa hatari kubwa kwa ulinzi wowote wa Ulaya, pamoja na Benardo Silva anayetegemewa kuwa muunganishi mkuu wa mashambulizi ya Madrid msimu huu.
Historia ya michezo ya karibuni pia inaonesha ubora wa Real Madrid, ingawa Espanyol waliwahi kuwashinda 1-0 msimu wa 2024/25 katika uwanja wao wa nyumbani. Shinikizo litakuwa kubwa kwa Mourinho kuanza vizuri katika ligi hii mpya, huku Espanyol wakitumaini kutumia fursa ya kucheza nyumbani na kasi ya Barcelona jirani kuwapa hamasa ya kuwashangaza mabingwa wa zamani wa Ulaya.

No comments:
Post a Comment