HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 19, 2026

PigaBet Yamshusha Thadei Kwenye Daladala, Sasa Afikia Wateja Kwa Wakati

Na Mwandishi Wetu

Dar es Salaam — Fundi wa mashine za photocopy kutoka Temeke, Mtega Thadei (33), sasa ana matumaini mapya ya kukuza kipato chake baada ya kushinda pikipiki kupitia kampeni ya #ShindaBoda ya PigaBet.

Kwa muda mrefu, Thadei alikumbana na changamoto ya usafiri wakati wa kuwafikia wateja wake, hali iliyokuwa ikiathiri kasi ya kazi na mapato yake. Akitumia daladala, mara nyingi alichelewa kufika kwa wateja na kupoteza fursa za kazi.

Akizungumza baada ya ushindi huo, Thadei alisema pikipiki hiyo itabadilisha namna anavyofanya kazi na kumwezesha kuwafikia wateja kwa haraka zaidi.

“Itanisaidia kuwafikia wateja kwa muda muafaka. Ilikuwa shida sana kufika kwa daladala, lakini sasa nitaweza kutoa huduma nzuri zaidi,” alisema.

Thadei, ambaye ni baba wa watoto watatu, alisema pia ushindi huo utamsaidia kuongeza kipato na kuboresha maisha ya familia yake.

“Kipato kitaongezeka, nitaweza ku-support familia yangu vizuri zaidi,” aliongeza.

Kampeni ya #ShindaBoda ya PigaBet inaendelea kutoa pikipiki kwa washindi kila wiki, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwapa wachezaji nafasi ya kushinda na kubadilisha maisha yao kupitia zawadi zinazoweza kuingiza kipato.

Kupitia ushindi huo, Thadei anaamini sasa ana nafasi ya kusukuma shughuli zake mbele kwa ufanisi zaidi na kujijengea msingi imara wa maisha.

18+ | Cheza kwa uwajibikaji

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad