Wafanyabiashara wa soko la CCM katika mamlaka ya mji mdogo wa Katoro halmashauri ya wilaya ya Geita wamelalamikia uhaba miundombinu ya kutiririshia maji machafu ambayo yanahatarisha afya zao.
Soko la Hilo ambalo linakadiliwa kuwa na wafanya biashara zaidi ya 400 ambao wanafanya biashara mbalimbali za nguo, vyombo, vyakula na pia linatajwa kuwa soko kuu la samaki katika mji huo wa Katoro.
Wafanyabiashara hao wamesema kuwa kutokana na uhaba wa miundombinu ya kupitishia maji taka maji hayo yamekuwa yakisambaa Kila mahali na kuleta harufu Kali.
Afisa afya katika halmashauri hiyo winner Mwansite amekili kufika katika soko Hilo mara kwa mara na kufanya ukaguzi lakini alikosa ushirikiano kutoka kwa mwekezaji wa soko Hilo ambapo Wahandisi wa mamlaka za maji walishauri kuchimba shimo kwa ajili ya kuhifadhi maji taka hayo
Kamati ya FEDHA na uchumi ya halmashauri ya wilaya ya Geita ilifika kukagua soko Hilo na kubaini uhaba wa miundombinu ya maji taka ambayo imekuwa kero kwa wafanyabiasha na wakazi wa maeneo jirani.
Kamati hiyo akiwemo mbunge wa Jimbo la Katoro injinia Kija Limbu Ntemi imemshauri Diwani wa kata ya Katoro kukaa chini na mwekezaji wa soko Hilo ili aweze kuchimba shimo ambalo litahifadhi maji taka hayo na kuondoa kero kwa wananchi na wafanyabiashara.
No comments:
Post a Comment