Akizungumza Jumatano Agosti 20, 2025 baada ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa jengo la 'Viwango House', Prof. Chande amenuagiza mkandarasi ambae ni kampuni ya CJIC kutoka nchini China kuongeza kasi ya ujenzi ili mradi huo ukamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
"Baada ya ukaguzi tumeridhika na ubora wa utekelezaji wa mradi huu, kwa sasa tunasisitiza mkandarasi aongeze kasi ili mradi ukamilike kwa wakati" amesema Profesa Chande.
Prof. Chande ameongeza kuwa ujenzi wa maabara na ofisi za TBS katika Kanda mbalimbali nchini ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha huduma inasogezwa karibu na wananchi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Katunzi amebainisha kuwa kukamilika kwa jengo hilo kutaondoa adha ya muda na gharama kubwa za kusafirisha sampuli kwa ajili ya vipimo kwenda Dar es salaam.
"Kwa sasa sampuli zinaenda katika maabara ya Dar es salaam lakini lengo ni kuwa na maabara katika Kanda na hivi karibuni tutakuwa na maabara Dodoma ambapo ujenzi umefikia asilimia 84 na Arusha tunatarajia kuanza ujenzi" amebainisha Dkt. Katunzi.
Kwa upande wake Meneja Mradi kutoka kampuni ya Kiota Architects, Arch. Chris Olomi amesema mradi umefika asilimia 47.7 ambapo ulianza mwaka 2024 ukitarajiwa kukamilika Aprili 04, 2026 kwa gharama ya shilingi bilioni 12 ikiwa ni jengo la ghorofa sita kwa kuanzia chini ya ardhi (ground floor).


Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi (TBS) Prof.Othman C. Othman(katikati)akiwa pamoja na wajumbe wa bodi wakati wa ziara katika mradi wa ujenzi wa jengo la Viwango House Mwanza.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi (TBS) Prof.Othman C. Othman(katikati)akiwa pamoja na wajumbe wa bodi wakati wa ziara katika mradi wa ujenzi wa jengo la Viwango House Mwanza.
No comments:
Post a Comment