Kampuni ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Mawasiliano Zanzibar (ZICTIA) wametia saini makubaliano ya ushirikiano (MoU) yenye lengo la kuharakisha mageuzi ya kidijitali Zanzibar na kupanua upatikanaji wa huduma bora katika visiwa hivyo.
Makubaliano hayo yaliyosainiwa katika hafla rasmi Zanzibar yanaweka mfumo wa kushirikiana kwenye miradi mikubwa ya miundombinu itakayoboreshwa upatikanaji wa huduma za intaneti ya kasi, kuongeza ujumuishi wa kidijitali na kuimarisha huduma za kijamii kupitia teknolojia.
Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini huo, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Zanzibar (WUMU), Mhe. Khalid Salum Mohammed alisema, “Ushirikiano huu kati ya Airtel Tanzania na ZICTIA ni hatua muhimu katika utekelezaji wa miradi ambayo itaongeza ujumuishi wa kidijitali kwa wananchi wetu.”
Aidha, Waziri alisisitiza umuhimu wa ubia kati ya sekta binafsi na ya umma akieleza kuwa, “Tunaamini katika ubia wa sekta ya umma na binafsi si kama sera tu, bali kama njia ya kivitendo ya kuharakisha e-serikali, e-elimu, e-afya na e-biashara, hasa katika maeneo ambayo hayajafikiwa vya kutosha.”
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. Charles Kamoto, alibainisha kuwa makubaliano hayo yanaendana na ajenda ya serikali ya kidijitali na malengo mapana ya ujumuishi wa kijamii na kiuchumi.
“Mkataba huu unaonyesha dhamira ya Airtel kuwa zaidi ya kampuni ya mawasiliano, tunawekeza kwenye miundombinu na ushirikiano unaowezesha jamii, kusaidia vipaumbele vya serikali na kuiweka Zanzibar kwenye njia ya ukuaji shirikishi na ubunifu,” alisema.
Mkurugenzi Mkuu wa ZICTIA, Mhandisi Shukuru Awadh Suleiman, naye alisema kuwa ubia huu unaonyesha nafasi kubwa ya ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi katika kufungua fursa za sekta ya TEHAMA Zanzibar.
“Kwa kupitia ushirikiano huu, tunapanua mtandao wetu wa miundombinu na kuunda jamii iliyounganishwa zaidi ambapo wananchi, wafanyabiashara na taasisi za serikali watanufaika na huduma za kidijitali zilizo salama, zenye uwezo mkubwa na za kuaminika,” alieleza.
MoU hiyo pia inalenga kukuza ujumuishi wa kifedha kwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha za kidijitali kwa wananchi.
Utiaji saini wa makubaliano haya unafungua ukurasa mpya kwa Airtel Tanzania katika nafasi yake ya kuwa nguzo muhimu ya maendeleo ya kidijitali Zanzibar. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa serikali, wawakilishi wa Airtel na ZICTIA pamoja na wadau wa sekta ya teknolojia na ubunifu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto (kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Zanzibar (ZICTIA), Mhandisi Shukuru Awadh Suleiman, wakisaini hati za makubaliano ya kimkakati ya uendelezaji wa huduma za kidigitali visiwani humo mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Meneja wa Sheria wa ZICTIA, Kassim Madai Kassim; Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano; Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar (WUMU), Dk. Habiba Hassan Omar; Waziri katika wizara hiyo, Khalid Salum Mohammed; Naibu Katibu Mkuu (WUMU), Hawah Ibrahim Mbaye, Ofisa Mkuu wa Ufundi Airtel, Prosper Mafole na Mkurugenzi wa Sheria Airtel, David Lema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto (wa tatu kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Zanzibar (ZICTIA), Mhandisi Shukuru Awadh Suleiman, wakishikana mikono mara baada ya kusaini hati za makubaliano ya kimkakati ya uendelezaji wa huduma za kidigitali visiwani humo mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano; Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar (WUMU), Khalid Salum Mohammed; Ofisa Mkuu wa Ufundi wa Airtel, Prosper Mafole na Mkurugenzi wa Sheria wa Airtel, David Lema.
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar (WUMU), Khalid Salum Mohammed akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto (kulia), katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya kimkakati ya uendelezaji wa huduma za kidigitali visiwani humo na Shirika la Mawasiliano Zanzibar (ZICTIA), mwishoni mwa wiki. Wengine kutoka kushoto ni, Mkurugenzi Mkuu wa ZICTIA, Mhandisi Shukuru Awadh Suleiman, Naibu Katibu Mkuu (WUMU), Hawah Ibrahim Mbaye na Katibu Mkuu katika wizara hiyo, Dk. Habiba Hassan Omar.
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar (WUMU), Khalid Salum Mohammed (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto, mara baada ya hafla ya utiaji saini makubaliano ya kimkakati ya uendelezaji wa huduma za kidigitali visiwani humo na Shirika la Mawasiliano Zanzibar (ZICTIA), mjini Zanzibar, mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto (katikati), akiagana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar (WUMU), Hawa Ibrahim Mbaye, mara baada ya hafla ya utiaji saini makubaliano ya kimkakati ya uendelezaji wa huduma za kidigitali visiwani humo na Shirika la Mawasiliano Zanzibar (ZICTIA), mjini Zanzibar, mwishoni mwa wiki. Kulia ni Ofisa Mkuu wa Ufundi wa Airtel, Prosper Mafole.
Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini huo, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Zanzibar (WUMU), Mhe. Khalid Salum Mohammed alisema, “Ushirikiano huu kati ya Airtel Tanzania na ZICTIA ni hatua muhimu katika utekelezaji wa miradi ambayo itaongeza ujumuishi wa kidijitali kwa wananchi wetu.”
Aidha, Waziri alisisitiza umuhimu wa ubia kati ya sekta binafsi na ya umma akieleza kuwa, “Tunaamini katika ubia wa sekta ya umma na binafsi si kama sera tu, bali kama njia ya kivitendo ya kuharakisha e-serikali, e-elimu, e-afya na e-biashara, hasa katika maeneo ambayo hayajafikiwa vya kutosha.”
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. Charles Kamoto, alibainisha kuwa makubaliano hayo yanaendana na ajenda ya serikali ya kidijitali na malengo mapana ya ujumuishi wa kijamii na kiuchumi.
“Mkataba huu unaonyesha dhamira ya Airtel kuwa zaidi ya kampuni ya mawasiliano, tunawekeza kwenye miundombinu na ushirikiano unaowezesha jamii, kusaidia vipaumbele vya serikali na kuiweka Zanzibar kwenye njia ya ukuaji shirikishi na ubunifu,” alisema.
Mkurugenzi Mkuu wa ZICTIA, Mhandisi Shukuru Awadh Suleiman, naye alisema kuwa ubia huu unaonyesha nafasi kubwa ya ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi katika kufungua fursa za sekta ya TEHAMA Zanzibar.
“Kwa kupitia ushirikiano huu, tunapanua mtandao wetu wa miundombinu na kuunda jamii iliyounganishwa zaidi ambapo wananchi, wafanyabiashara na taasisi za serikali watanufaika na huduma za kidijitali zilizo salama, zenye uwezo mkubwa na za kuaminika,” alieleza.
MoU hiyo pia inalenga kukuza ujumuishi wa kifedha kwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha za kidijitali kwa wananchi.
Utiaji saini wa makubaliano haya unafungua ukurasa mpya kwa Airtel Tanzania katika nafasi yake ya kuwa nguzo muhimu ya maendeleo ya kidijitali Zanzibar. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa serikali, wawakilishi wa Airtel na ZICTIA pamoja na wadau wa sekta ya teknolojia na ubunifu.
No comments:
Post a Comment