HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 14, 2025

OKTOBA KAZI NI MOJA TU,TUSIMAME NA RAIS SAMIA TUMUUNGE MKONO KWA VITENDO - NAMELOCK

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,Ndugu Namelock Edward Sokoine, amepokelewa kwa hamasa,nderemo, vifijo  na umati wa Wananchi leo Jumamosi Juni 14,2025 mkoani Arusha, alipowasili kwa ziara ya kikazi.

Ndugu Namelock alieonekana kuwa na furaha kubwa baada ya kushuhudia mapokezi makubwa kutoka kwa Wananchi wa Arusha,akapata wasaa wa kupanda jukwaani na kuhutubia maelfu ya wakazi wa Wilaya Monduli na Viunga vyake ndani ya jiji la Arusha .

"Namshukuru kwa dhati ya moyo wangu Mwenyekiti wangu wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa heshima kubwa aliyoitoa kwa Mkoa wa Arusha kupitia nafasi ya Uongozi niliyonayo kwa sasa,

Kwa niaba ya wana-Arusha na Monduli kwa ujumla, naahidi kuitunza na kuilinda heshima hii kwa moyo wote,na ninawaomba tuendelee kumuombea na kumuunga mkono Rais wetu kwa mambo mbalimbali ya kimaendeleo anayoyafanya ndani ya nchi yetu,” alisema Ndugu Namelock  kwa msisitizo.

Aidha, Ndugu Namelock aliwahimiza wananchi kujiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao kwa kusema: “Oktoba kazi ni moja tu, tusimame na Mama Samia, tumuunge mkono kwa vitendo ili kuendeleza maendeleo yanayoonekana kote nchini,na kwamba ahadi ya watu wa Monduli ni ile ile 2025 kura zote kwa Mhe.Rais Dkt Samia na Mgombea Mwenza Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi.

Ndugu Namelock pia alimaliza kwa kuweka msisitizo kuwa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia umeendelea kuleta matumaini, mshikamano na dira ya maendeleo kwa Watanzania wote, hivyo kuna kila sababu ya kuendeleza mshikamano  ndani ya chama na kwa Taifa.









No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad