HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 9, 2025

USIKUBALI KUKAMATWA NA MTU YEYOTE BILA KUONYESHWA KITAMBULISHO - RPC GEITA

Wananchi wametakiwa kutokubali kukamatwa na mtu yeyote anaedai kuwa ni askari polisi bila ya kuonyesha kitambulisho kutokana na matukio ya utekaji yanayodaiwa kufanywa na watu wanaovaa sare za polisi. 

Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita Safia Jongo ametoa kauli hiyo wakati wa mafunzo ya ulinzi shirikishi na polisi jamii, yaliyotolewa kwa watendaji wa kata, vijiji, mitaa,wenye viti na maafisa tarafa, yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGML) kwa lengo la kuimarisha usalama wa wananchi kupitia ushirikiano wa karibu. 

Jongo amesema wananchi wana haki ya kuuliza na kutaka uthibitisho kabla ya kukubali kuchukuliwa au kupekuliwa, na kwamba mtu yeyote anayeshindwa kujitambulisha hana mamlaka ya kumkamata raia. 


Mtendaji wa Kata, Martin Matiba amesema mafunzo hayo yamewawezesha watendaji kupata uelewa mpana wa namna ya kushirikisha jamii katika masuala ya ulinzi bila kuvunja sheria, huku wakitakiwa kuhamasisha wananchi kuachana na tabia ya kujichukulia sheria mkononi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad