HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 8, 2024

TET YAINGIA MAKUBALIANO NA SHIRIKA LA EDUCATE KUTOA MAFUNZO KWA WALIMU WA MASOMO YA BIASHARA

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imeingia makubaliano ya Ushirikiano na Shirika lisilo la Kiserikali la 'Educate', katika kuimarisha utoaji wa mafunzo endelevu kwa walimu mashuleni hasa katika somo la biashara na kuwawezesha kufundisha somo hilo kwa kutumia mbinu za kisasa na kuwa na maarifa yanayoendana na wakati katika ufundishaji.

Akizungumza katika hafla hiyo leo Julai 8,2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu TET, Dkt. Aneth Komba amesema makubaliano hayo yanakwenda kuwezesha TET kuwa kitivo cha utafiti utakaosaidia kukuza na kubadilishana uzoefu na ujuzi katika utekelezaji wa mafunzo ya somo la biashara, pamoja na kumuandaa mtanzania anaeweza kushindana kimataifa.

Amesema makubaliano hayo yatasaidia katika maandalizi ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia kama vile vitabu, kiongozi Cha mwalimu, na vifaa vingine katkka ngazi ya sekondari hatua ya chini kwa somo la elimu ya biashara.

"Educate katika eneo hili wanatusaidia kutoa utaalamu lakini pia kutoa rasilimali fedha" amesema Dkt. Aneth.

Aidha, amesema kuwa mtaala mpya ulioboreshwa umeanza utekelezaji wake rasmi mwezi huu kwa kidato cha tano na elimu ya ualimu Stashahada, na kwamba TET wamejipanga vizuri kuhakikisha maandalizi ya kutoa mafunzo kwa walimu pamoja na vifaa vya ufundishaji vinakuwepo.

Amesema mtaala uliyoboreshwa ambao unatekelezwa kwa sasa unatokana na sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023, ambalo linasisitiza umuhumu wa ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo kutoa elimu bora kwa ngazi zote nchini.

"Educate wamekuja wakati muafaka wakati tunaendelea na utekelezaji wa mitaala iliyoboreshwa, ambayo jambo kubwa ni kuanzishwa kwa somo jipya la biashara ambalo ni la lazima ngazi zote za elimu," amesema Dkt. Aneth.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Educate, Kamanda Kamiri, amesema kuwa safari ya ushirikiano baina yao ilianza mwaka 2022 nchini Rwanda ambapo ilikuwa safari ya mafunzo.

Amesema kuwa kwa kuanza wameanza na masomo ya biashara lengo likiwa na kuwatengenezea wanafunzi mazingira ya kuongeza ujuzi zaidi katika Sekta ya biashara ili kukuza soko la ajira kupitia kujiajiri wenyewe baada ya kuhitimu masomo.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) , Dkt. Aneth Komba akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Educate, Kamanda Kamiri wakisaini makubaliano ya ushirikiano katika kuimarisha utoaji wa mafunzo endelevu kwa walimu mashuleni. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 8,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba akibadilishana mikataba na Mkurugenzi wa Shirika la Educate, Kamanda Kamiri mara baada ya kusaini makubaliano ya ushirikiano katika kuimarisha utoaji wa mafunzo endelevu kwa walimu mashuleni. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 8,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) , Dkt. Aneth Komba akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Educate, Kamanda Kamiri wakionesha mikataba waliosaini ya makubaliano ya ushirikiano katika kuimarisha utoaji wa mafunzo endelevu kwa walimu mashuleni. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 8,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) , Dkt. Aneth Komba akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini ya makubaliiano ya ushirikiano katika kuimarisha utoaji wa mafunzo endelevu kwa walimu mashuleni. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 8,2024 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Shirika la Educate, Kamanda Kamiri akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini ya makubaliiano ya ushirikiano katika kuimarisha utoaji wa mafunzo endelevu kwa walimu mashuleni. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 8,2024 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) , Dkt. Aneth Komba akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Educate, Kamanda Kamiri wakipata picha ya pamoja na watumishi wa TET pamoja na watumishi wa Educate wakati wa hafla ya utiaji saini ya makubaliiano ya ushirikiano katika kuimarisha utoaji wa mafunzo endelevu kwa walimu mashuleni. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 8,2024 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad