HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 21, 2024

Airtel Tanzania yaahidi uhusiano imara na vyombo vya habari vya Tanzania

 



KAMPUNI ya Airtel Tanzania inaendelea kushirikiana na tasnia ya nchini kwa ufadhili wa hivi karibuni wa Mkutano wa Kitaifa wa Maendeleo ya Sekta ya Habari uliohudhuriwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi.

Katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Rais Samia alivipongeza vyombo vya habari kwa mchango wake mkubwa wa kuhabarisha umma juu ya hali ya maendeleo nchini.

“Vyombo vya habari vinafanya kazi kubwa kuhabarisha, kuelimisha na kuamsha jamii kuhusu mambo muhimu. Na kupitia kwao, serikali inapata kujua na kukusanya maoni ya umma kuhusu masuala mbalimbali. Sekta hii inahamasisha upatikanaji wa ujuzi mpya na maendeleo ya teknolojia kwa ustawi wa jamii zetu. Vyombo vya habari pia vinachangia kujenga uwajibikaji ndani ya sekta ya umma,” alisema.

Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Airtel Tanzania, Beatrice Singano, alieleza kuwa vyombo vya habari ni sekta muhimu inayoendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sekta ya mawasiliano na kutumia nguvu ya teknolojia kupitia majukwaa ya kidijitali.

"Vyombo vya habari vinasaidia kwa nafasi kubwa katika ukuaji wa maendeleo ya sekta tofauti. Ni sekta inayotoa taarifa kwa umma kuhusu bidhaa zetu ambazo zimeundwa kukuza maendeleo na ushirikishwaji wa kifedha lakini pia, inaonyesha mwelekeo wa sekta hii katika kiwango cha kimataifa," alielezea.

Aliongeza zaidi “Hivi majuzi tulizindua mradi wetu mkukwa unaoitwa Airtel SMARTWASOMI ambao umeundwa kushirikiana na serikali kukuza ujuzi na viwango vya wasomi wetu walioko shule za sekondari kuwa na uwezo wa kuja kufanya mambo mengi kidijitali. Tusingeweza kufikia shule nyingi kama tulivyofanya bila ushirikiano wa vyombo vya habari. Tutaendelea kusaidia sekta ya vyombo vya habari kwa njia bora tuwezavyo.”

Singano aliendelea kusema kwamba Airtel Tanzania imejizatiti kuimarisha na kupata mawasiliano kufuatia uanzishaji wa hivi karibuni wa Mkongo unaopita chini ya bahari wa 2Africa, ambao inaipa sekta ya kidijitali sura mpya ya maendeleo.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad