HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 5, 2024

TUME YA TAIFA YA UNESCO :HARAKISHENI MCHAKATO WA KUINGIZA ORODHA YA HIFADHI ZA DUNIA

 

Mkuu wa Progamu za Urithi wa Dunia wa Tume ya Taifa ya UNESCO Eric Kajiru akiwasilisha mada katika Semina ya wadau Maeneo ya Hifadhi za Asili ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Urithi wa Dunia Afrika yaliyofanyika Kitaifa wilayani Kondoa mkoani Dodoma


*Yataka wadau watumie fursa hiyo kabla ya vigezo havijabadilika

Na Mwandishi Wetu
TUME ya Taifa ya UNESCO Tanzania imewataka wadau ambao wanataka kuziingiza maeneo yao katika orodha urithi wa dunia kuanza mchakato kabla ya 2027 kwani huenda taratibu zikabadilika na kuwa ngumu zaidi.

Akiwasilisha mada kwa wadau wa maeneo ya hifadhi za asili na utamaduni katika maadhimisho ya siku ya Siku Uridhi wa Dunia Afrika yaliyofanyika Kitaifa wilayani Kondoa mkoani wa Dodoma, Mkuu wa programu za Urithi wa Dunia wa Tume Eric Kajiru amesema hivi sasa mchakato unaruhusu kuingiza hata sites 4 kwa wakati mmoja tofauti na utaratibu unaopendekezwa wa nchi kuwa na pendekezo la site moja kwa wakati mmoja.

Kajiru amesema Tanzania ina vivutio vingi vyenye sifa ya kuwa na hadhi hizo lkn kumekuwa na uzito katika kuanzisha mchakato jambo ambalo linalirudisha nyuma taifa.

Akizunguzia utayarishaji wa wasilisho la kutaka kutambulika na kuingizwa kwenye orodha ya urirhi wa dunia Kajiru amewataka wadau wahakikishe wanawashirikisha wadau wote wanaohusika ktk maendeleo ya maeneo yao ili kurahisisha mchakato na kuweka vipengele vya maangalizo iwapo eneo husika litahitajika ktk shughuli ingine.

Kuhusu mchango wa tume ya taifa kufanikisha hilo, Kajiru amesema tayari kuna baadhi ya maeneo ambayo yako katika hatua mbalimbali za kuandaa mawasilisho na kuwataka wadau wasisite kuwasiliana Tume pindi wanapohitaji muongozo na msaada unaolenga kufanikisha mchakato huo.

Ametoa mfano wa walipokuwa wakiingiza hifadhi ya Selous katika orodha mwaka 1982 watayarishaji walieleza kuwa serikali inampango wa kujenga Bwawa jambo ambalo lilisaidia kupitishwa kwa mradi huo kirahisi wakati ambao wanaharakati walitaka kuzuia lakini sasa umetekelezwa

Hivi sasa Tanzania ina maeneo ya Saba ya Uridhi Dunia ambazo ni Hifadhi ya Ngorongoro, Mji Mkongwe Zanzibar, Magofu ya Kilwa Songo Mnara na Kilwa Kisiwani, Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, Michoro ya asili ya Irangi Kondoa pamojà na Hifadhi ya Serengeti.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad