HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 20, 2024

Makamu wa Pili wa Rais Z'bar Atoa Wito wa Kuulinda Muungano

 MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla ametoa wito kwa wananchi wa Tanzania kuendelea kuulinda Muungano.


Hayo ameyasema leo Aprili,19,2024 jijini Dar es Salaam katika maonesho ya Taasisi za kimuungano ambapo amesema kuwa huwezi kuutenganisha umoja wa Watanzania wale wa Visiwani na Bara kwa kuwa tayari watu hawa wameungana kwa damu.

"Tangu enzi za wazee wetu watu wa visiwani wanaishi bara, wameoa bara wamejukuu bara hivyo hivyo wa bara wanaishi na wale wa bara wanaishi visiwani wameona, wamejukuu watu hawa huwezi kuwatenganisha" alisema Makamu wa pili wa Rais.

Amesema kuwa amefarijika kuona maonesho yaliyoandaliwa na Taasisi za kimuungano na kuwataka wananchi kufika kwenye maonesho hayo ili kujifunza zaidi kuhusu muungano.

Amesema kuwa Muungano umeimarika zaidi husasani kwenye huduma za kijamii na uchumi "kauli mbiu ya mwaka huu tumeimarika na tumeshikamana kwa maendeleo ya taifa letu tutaendelea umoja wetu, Muungano wetu ".

Amesema kuimarika kwa mahusiano kumetoa fursa kwa wafanyabiasha wa pande zote mbili kuwekeza katika nyanja mbambali.

Ametoa wito wa kuulinda Muungano ili kuitunza Tunu hiyo muhimu iliyotimiza miaka 60 .

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis amemhakikishia Makamu wa Pili wa Rais kuw muungano upo salama.
"Sisi wanadar es Salaam tunayomengi ya kuzungumzia kuhusu Muungano na haya maendeleo yanayoonekana hapa ni zao la Muungano."

Amesema kuwa muingiliano wa biashara umekuwa mkubwa watu wanafanya shughuli zao na wanatembea kila upande wa Muungano bila kuwa na hati kusafiria "Utawaona wapo Darajani kule Zanzibar utawaona Kariakoo hapa Dar es salaam huwezi kuwatofautisha".

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cypran Luhemeja
,amesema Muungano huu umetupa fursa za kibishara na za kujamii "wengine tumepata fursa ya kuchanganya damu kwa maana tumeoa Zanzibar"
Amesema kuwa uchumi umekuwa kutokana kuchagizwa na ushirikiano wa kibiashara.

Amesema kuwa tayari Serikali ya Jamhuri imeshughulikia changamoto takribani zote za muungano.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akifungua Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akitoa salamu wakati wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa neno la ukaribisho wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
  
Washiriki mbalimbali wakifuatilia ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad