HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 9, 2024

AMEND, USWISI WAPELEKA ELIMU USALAMA BARABARANI KWA BODABODA WILAYANI MUHEZA

 

Na Mwandishi Wetu,Muheza

MADEVERA wa bodaboda wilayani Muheza mkoani Tanga wameeleza namna ambavyo wamekuwa sehemu ya vyanzo vya ajali za barabara kutokana na ukosefu wa  elimu ya usalama barabara miongoni mwao.

Wakizungumza wakati wa kampeni ya kutoa elimu ya  ya usalama barabara katika eneo la Mkanyageni barabara kuu ya Tanga Segera iliyoendeshwa na kikosi cha usalama barabara kwa kushirikiana na Shirika la Amend kupitia ufadhili Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania.

Madereva hao wa bodaboda wamesema kuwa wengi wao wamejifunza uderava wa vyombo hivyo  mitaani bila ya kwenda darasani kupata elimu sahihi hatua ambayo imekuwa ikiwasababishia wao kuwa visababishi vya ajali za barabara 

Dereva bodaboda Meshark Mhando amesema licha ya kazi hiyo kuwasehemu ya vipato vyao  lakini changamoto iliyokuwepo hawana elimu ya usalama barabara.

"Tunashukuru kwa hii kampeni ya mafunzo ya usalama barabarani kwanihii imeweza kutupatia mwangaza wa umuhimu wa kuwa na elimu ya usalama barabara hususani katika matumizi ya vyombo vya moto uwepo barabarani,"amesema.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Muheza mkoani Tanga Herberth Kazonde  amesema kwamba  ufadhili huo wa ubalozi wa Uswizi kupitia shirika la Amend elimu hiyo wanayoitoa itawasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali pamoja na makosa mbalimbali ya barabara yanayoweza kuzuilika.

Amefafanua kupitia kampeni hiyo wanayoitoa ni imani yao kama kikosi cha usalama barabara kuhakikisha bodaboda wanakuwa kundi salama kwani Sasa litakuwa na watu ambao ni waelewa tofauti na hapo awali .

"Kampeni hii tayari imeanza kuleta matunda katika maeneo ambayo elimu imeshafika kwani makosa ya barabara yameweza kupungua kwa kiwango cha kuridhisha hivyo tunawashukuru ubalozi wa Uswizi kwa kuja na mradi huu wa Elimu ya usalama kwa kundi hili la bodaboda"alisema.

Wakati huo huo  Mratibu wa mradi huo kutoka shirika la Amend Ramadhani Nyaza amesema kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi waliona wapeleke kampeni hiyo katika eneo la Mkanyageni kwani limeoneka ni hatarishi kwa ajali za barabara 

"Tumekuja kutoa elimu ya usalama barabara ambapo tumewafundisha umuhimu wa wao kuhakikisha wanakuwa salama muda wote wanapotumia vyombo vya moto lakini na kuzingatia usalama wa watu wengine wanaotumia barabara hizo,"amesema  Nyaza.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad