HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 1, 2024

MVUA ZAHARIBU DARAJA LA NAMIUNGO TUNDURU,WATAALAM WA TANROADS MKOA WA RUVUMA YAPIGA KAMBI

 

sehemu ya daraja katika mto Namiungo wilayani Tunduru ambalo limeharibika na mvua zilizonyesha kwa wingi katika kijiji hicho na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu pamoja na mazao kusombwa na maji.
Meneja wa wakala wa barabara(TANROADS)mkoa wa Ruvuma Mhandisi Saleh Juma,akionyesha sehemu ya daraja la mto Namiungo ambalo limeharibika vibaya kwa kukatika upande mmoja wa daraja hilo kutokana na mvua kubwa iliyonyesh kwa zaidi ya masaa manne.
Baadhi ya magari yakianza kupita upande mmoja wa darala katika mto Namiungo wilayani Tunduru kufuatia upande mmoja wa daraja hilo kusombwa na maji ya mvua.

Na Mwandishi wetu,
Tunduru


MVUA kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha kwa zaidi ya masaa manne katika kijiji cha Naminungo wilayani Tunduru imeharibu miundombinu ya daraja la mto Namiungo lililopo Barabara kuu ya Tunduru kuelekea mikoa ya kusini Lindi,Mtwara na mikoa ya Pwani na Dar es slaam.


Meneja wa wakala wa Barabara mkoani Ruvuma Mhandisi Saleh Juma alisema, mvua hiyo imekatika upande mmoja wa daraja na kusababisha adha kubwa kwa watumiaji hasa magari makubwa na madogo yanayopita katika barabara hiyo.


Alisema,kuharibika kwa barabara hiyo kumepelekea magari kupitia upande mmoja kwa shida,hata hivyo tayari Tanroads haimechukua hatua kwa kumpeleka mkandarasi katika eneo hilo kwa ajili ya kurejesha miundombinu iliyoharibika.


Alisema,kazi wanayoifanya kwa sasa ni kuhakikisha wanakata upande mmoja ulioharibika na kufanya matengenezo makubwa ya kurudisha hali yake ya awali ili kuruhusu shughuli za kiuchumi ziweze kuendelea.


Kwa mujibu wa Saleh ni kwamba,baada ya mvua kupungua watafanya tathimini ya kina katika daraja hilo ili kujua kama kuna ulazima wa kuongeza mdomo mwingine wa kupitisha maji au wazidi kuimarisha miundombinu.



Amewatahadharisha wananchi wanaofanya shughuli za kilimo kando kando ya mto huo kuacha mara moja shughuli zao, kwani kwani kwa sasa maeneo hayo siyo rafiki kwao ili kuepuka madhara makubwa na hasara kwa mazao yao kusombwa na maji.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Namiungo walisema,hali hiyo imetokana na mvua kubwa iliyonyesha katika kijiji hicho ambayo haijawahi kutokea kwa takribani miaka hamsini.


Nora Abdala alisema,maji yalikuwa yanapita juu ya daraja na kusomba miundombinu yake hali iliyosababisha magari kusimama kwa muda kabla ya kuendelea na safari zake baada ya maji kupungua katika eneo hilo.


Mohamed Makota alisema, kwa muda mrefu hawajawahi kushuhudia mto Namiungo ukijaa maji mengi kwa kiwango hicho,ambapo ameishauri serikali kupitia wakala wa barabara Tanroads kuchukua hatua ya haraka kurejesha miundombinu katika daraja hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad