HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 8, 2024

Malazi ya Hifadhi ya Mikumi Sawa na Bure

 

Mkuu wa Hifadhi ya Mikumi Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi Agustine Masesa akizungumza na waandishi habari katika Hifadhi ya Mikumi ,Mkoani Morogoro .


*Mkuu wa Hifadhi anena mambo manne ya kuvutia watalii wa Ndani.

Na Mwandishi Wetu HIFADHI ya Mikumi imesema kuwa watanzania kutalii hifadhi pamoja na kupata malazi katika hifadhi hiyo ni gharama shilingi 23000.

Hayo ameyasema Mkuu wa Hifadhi ya Mikumi Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi Agustine Masesa wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo.

Watanzania wamekuwa wakifikifiria kufanya utalii katika hifadhi hiyo ni gharama kubwa ambapo Hifadhi hiyo imeweka mazingira rafiki ya kila mtanzania kufanya utalii katika hifadhi ya Mikumi kutokana na kuwa na miundombinu rafiki ikiwemo Barabara ya lami pamoja na Reli pamoja na Ndege

Masesa amesema Hifadhi ya Mikumi ndio hifadhi inayoongoza kwa idadi kubwa ya watalii wa ndani kutokana na Jiographia yake ya Kufikika kwa urahisi.

Amesema kuwa katika hifadhi ya Mikumi kwa mtalii wa ndani kupata huduma ya chakula ndani ya hifadhi kwa sh.2000 lengo ni kila mtanzania kufanya utalii katika hifadhi hiyo kiwango kidogo cha kiingilio cha 5000.

Mkuu wa Uhifadhi Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi Masesa Amesema kuwa wamejipanga kuona watanzania wanavutika kutembelea hifadhi hiyo na kuona vivutio vingi ambavyo adimu katika hifadhi hiyo.

Hata hivyo amesema wanyama wanaopatikana katika hifadhi hiyo ni Simba ,Tembo, Chui ,Faru pamoja na Tembo huku kukiwa na wanyama wengine wengi ukiachana wanyama wa Big Five

Amesema kuwa wakati umefika kwa kika mtanzania kuwa katika mipango yao ni pamoja na kufanya utalii katika hifadhi ya Mikumi.

Amesema kuwa unaweza kutalii hata kwa magari binafsi katika hifadhi hiyo bila kutumia magari ya kukodi kutembezwa.

Masesa amesema watanzania waunge jutihada za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika filamu ya Royal Toure nao kutembelea hifadhi ya Mikumi.

Amesema Hifadhi hiyo ina vivutio vya aina yake ambayo huwezi kuona katika hifadhi nyingine hivyo watanzania wakitaka kujua asili yao kutembelea Mikumi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad