HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 22, 2024

MTANDAO WA WANAWAKE, KATIBA, UONGOZI NA UCHAGUZI WATOA TAMKO

 Na Karama Kenyunko Michuzi Tv

MTANDAO wa Wanawake, Katiba, uchaguzi na Uongozi nchini umeiomba kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhakikisha suala la misingi ya usawa wa kijinsia linawekwa katika miswada mitatu iliyowasilishwa Bungeni.

Miswada hiyo ni mswada wa sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, 2023 ,mswada wa Marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa 2023 na Mswada wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi 2023.

Akizungumza na waandishi wq habari Jijini Dar es salaam leo Januari 22, 2024 wakati wa kutoa tamko hilo, Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uongozi, Mary Ndaro, amesema mtandao huo baada ya kufanya uchambuzi yakinifu wa miswada yote mitatu imegundua uwepo wa mapengo ya Jinsia katika miswada hiyo.

"Kwa pamoja tunadai mabadiliko katika miswada hii Ili kuweza kuwa na Sheria zenye mrego wa Jinsia na zenye kuweka misingi ya uwajibishwaji Kwa wale wote wenye dhamana ya kusimamia na kutekeleza Sheria husika"amesema na kuongeza kuwa,

" Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linayoongozwa na Spika mwanamke, ikiwa ni Taasisi nyeti kwenye kutunga Sheria, ipokee maoni yetu na kuyaingiza kwenye maboresho ya miswada hii mitatu".

Ndaro amesema mtandao huo umeamua kuja na mapendekezo ambayo ni mswada wa uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2023 sura ya tatu kifungu cha 32 ubainishe usawa wa jinsia (50/50) Kwa kuvitaka vyama vyote vyenye nia kushindania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania viteue wagombea wawili mgombea kitu Cha Urais na makamu wake.

Pia wamependekeza mabadiliko ya kisheria yatakayowezesha kufikia uwakilishi wa 50/50 Kwa njia ya majimbo ya uchaguzi ili wanawake wapigiwe kura na wapiga kura wote badala ya kuviacha vyama vya siasa kutumia au kugeuza haki za wanawake kwenye kuteuliwa kama jambo la hiari au hisani.

Vilevile amesema majimbo ya uchaguzi yagawanye upya kwa kuzingatia wingi wa watu na sio kijiographia na kueleza kuwa yote hayo yatawezekana endapo mswada wa sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani sura ya sita itafanyiwa mabadiliko makubwa.

Aidha ameongeza kuwa, mswada wa Marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa,2023 hauwajibishi vyama kuzingatia misingi ya usawa kwenye uteuzi wa wagombea Wala kuwajibisha vyama kutenga mfuko maalumu wa kuwezesha utekelezwaji wa sera ya jinsia na haviwajibishi vyama kuwa mfumo wa uwazi kwa kuzingatia Utawala Bora na wazi kwa mrego wa jinsia.

Kwa upande wa Mswada wa sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi 2023 haukubainisha Msingi wa usawa wa jinsia, haukuzingatiwa katika kuongeza teuzi za watendaji wakuunna katika kuunda kamati mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad