HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 1, 2023

TRA YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KITUO CHA AFYA CHA WANAWAKE NA WATOTO

 

Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Charangwa Selemani, akikabidhi kwa Kaimu Mganga wa Jiji la Dar es Salaam, Dk.Gerwalda Mumba msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni saba, katika Kituo cha Afya cha Mama na Mtoto, Chanika, Nguvu Kazi, vilivyotolewa na Mkoa wa Ilala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Mlipakodi. Wa pili kulia ni Kaimu Mganga wa Jiji la Dar es Salaam, Dk.Gerwalda Mumba na kulia ni Mganga Mfawidhi wa kiyuo hicho, Dk. Hezron Ruyange.
Meneja wa Walipakodi Mkoa wa Ilala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Masau Malima, akikabidhi kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Charangwa Selemani, msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni saba, katika Kituo cha Afya cha Mama na Mtoto, Chanika, Nguvu Kazi, ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Mlipakodi. Wa pili kulia ni Kaimu Mganga wa Jiji la Dar es Salaam, Dk.Gerwalda Mumba na kulia ni Mganga Mfawidhi wa kiyuo hicho, Dk. Hezron Ruyange.



MAMLAKA ya mapato Tanzania ( TRA) imekabidhi vifaa tiba katika kituo cha Afya cha Mama na Mtoto cha Nguvukazi kilichopo Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa mamlaka hiyo kutoa shukrani kwa mlipa kodi.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa vifaa hivyo leo Desemba Mosi, 2023, DAS wa Manispaa ya Ilala Charangwa Selemani amezitaka Taasisi na Mashirika mbalimbali kujitoa kwa jamii hasa katika vituo vya afya vyenye uhitaji zaidi vilivyo pembezoni mwa mji na vyenye wagonjwa wengi ili kupunguza changamoto mbali mbali za Afya zinazowakabili.

Amesema, TRA wamefanya matendo ya huruma, kwani wanakusanya kodi kwa jamii na kuwarudishia wema kwani vifaa tiba walivyokabidhi leo na bidhaa nyinginezo ni neema kwa kituo hicho cha afya cha Nguvu kazi.

Aidha amewashukuru TRA kwa kutoa msaada huo wa vifaa hivyo kwani kwa kufanya hivyo wanaendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

"Tunashukuru sana TRA kwa kuweza kukiona kituo hiki Cha Chanika ambacho kipo pembezoni kabisa ya mji, ni kituo Cha Afya lakini kinabeba wananchi wengi, wakazi wengi wa Wilaya ya Ilala ni wakazi ambao wanakaa katika Kata hii ya Chanika, Zingiziwa, Msongola na Gongolamboto ambao wengi wanakitegemea kituo hiki Cha Chanika"

Pia amewataka TRA kuendelea kukusanya mapato na kufanya maendeleo ili kufikia malengo.

Kwa upande wake Meneja wa Mkoa wa Kodi wa Ilala, Masau Malima amesema jumla ya vifaa walivyopeleka katika hospitali hiyo vina thamani ya Shilingi 7.6 ambapo miongoni mwa fedha hizo zipo ambazo zimetoka mifukoni mwa watumishi wa TRA Ilala na Mfuko wa Mkoa.

"Hata mtumishi mmojammoja ameguswa kwa namna ambavyo anaweza akachangia maisha ya mama na mtoto"

Aidha Malima amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa maelekezo thabiti kwa TRA maelekezo ya baraza la mawaziri ambayo kwa kiasi kikubwa yameendelea kuimarisha hali ya uchumi, ukusanyaji kodi na kuongezeka kwa Kasi kubwa kwa mapato ya serikali kwa ujumla.

Kadhalika Malima aliwataka wale wote wanaotakiwa kulipa mapato yao kulipa mapato hayo kabla ya tarehe 31 Desemba mwaka huu.

Naye Mganga mfawidhi wa kituo hicho, Dkt. Hezron Liyange, ameishukuru serikali kwa kuwawezesha TRA kuweza kuwapatia vifaa hivyo ingawa bado wanauhitaji mkubwa wa vifaa hivyo kwani wanatarajia kuongeza wodi ya watoto wachanga.

"Kwa siku wagonjwa wanaowahudumia kituoni hapa ni 200-300 huku upande wa akina mama wanaojifungua ni 40-100.... kwa mwezi wakina mama pekee wanaoingia wodi ya wazazi ni 700-1000 na wanaojifungua hapohapo ni 800-900 lakini pia wapo watoto robo tatu yao wanahitaji huduma za dharura kutokana na kuwa na changamoto kadhaa hivyo imepeleka uhitaji wa vifaa kuwa mkubwa Hospitalini hapo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad