HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 4, 2023

MAMA LISHE WOTE WILAYA YA RUFIJI WAPATIWA MITUNGI YA GESI YA ORYX

 

 Na Mwandishi Wetu,

MBUNGE wa jimbo la Rufiji mkoani Pwani ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa kwa kushirikiana na Oryx Gas Tanzania amegawa mitungi gesi 900 yakiwa na majiko yake kwa Mama Lishe wote wa Wilaya ya Rufiji, lengo likiwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Ugawaji huo wa mitungi ya gesi ya Oryx umefanya wakati tayari Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amezindua Mpango wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa Wanawake wa Bara la Afrika.

Akizungumza wakati wa kugawa mitungi hiyo kwenye Wiki ya kukumbuka mchango wa Bibi Titi Mohamed ambaye enzi za uhai wake ametoa mchango mkubwa katika kulikomboa Taifa hili ambapo Waziri Mchengerwa na Oryx wameona iko haja kuwakumbuka Mama Lishe wa Rufiji kwa kutambua mchango wao katika kuinua uchumi wao na Taifa kwa  ujumla sambamba na utunzaji mazingira.

Wakati anazungumza Mchengerwa amesema matumizi ya kuni na mkaa yamekuwa yakichangia uharibifu wa mazingira na kusababisha kero mbalimbali nchni, hivyo kutumia nishati safi ya kupikia kutapunguza uharibu wa maazingira lakini pia kulinda afya za wanawake na watoto ambao ndio waathitika wakubwa wa moshi wa kuni wakati wa kupika.

"Tunatambua mchango mkubwa wa kundi hili la mama zetua na dada zetu ambao wanajihusisha na shughuli za Mama Lishe, hivyo kwa kushirkiana na viongozi wenzangu wakiwemo madiwani tulikubabaliana tutafute mitungi ya gesi ya orxy na kisha kuwapatia mama lishe wote wa wilaya ya Rufiji ambao idadi yao ni  1300 .

"Hivyo leo kwa kushirikiana na Kampuni ya Oryx tunagawa bure mitungi 900 yakiwa na majiko yake bure na mitungi iliyobakia tutagwa hivi karibuni.Tunataka kuona Mama Lishe wa wilaya ya Rufiji wanakuwa sehemu ya kutunza mazingira kwa kupikia nishati safi...

"Lakini wakati huo huo kuwalinda dhidi ya athari zinazotokana na kuvuta moshi wa kuni wakiwa katika shughuli zao za kila siku,”amesema Mchengerwa huku akisisitiza  umefika wakati wa wananchi kuungana na Serikali inayoongozwa na Rais Samia kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Benoit Araman amesema wamefurahi kupeleka nishati safi ya kupikia kwa wananchi wa wilaya ya Rufiji na kugusa kundi hilo muhimu katika jamii ambalo shughuli zao za kila siku zinahitahi kupata nishati ya kupikia.

“Kupika katika gesi ya oryx ni kulinda mazingira kwa kuacha kukata miti na zaidi ya yote ni kulinda afya ya wanawake na watoto ambao wamekuwa wakiathirika kwa kuvuta moshi mbaya unaotokana na kuni. Rais wetu Mama Samia amejipanga kuhakikisha wananchi wote nchini wanapata nishati safi ya kupikia ifkapo 2032.

“Katika mkutano wa Dubai ,Rais Samia amezindua Mpango wa Nishati safi ya kupikia kwa wanawake wa Afrika.Oryx Gas tutaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhamasisha matumizi ya nishati safi ua kupikia kwa kugawa bure mitungi ya gesi na majiko yake.

“Hadi leo hii Oryx tunajivunia kwa kutoa mitungi zaidi ya 15000 yenye thamani ya zaidi ya Sh.bilioni moja katika kipindi cha kuanzia mwaka 2022 mpaka sasa kupitia mpango wetu wa kuhamasisha nishati safi ya kupikia ikiwa ni sehemu ya kuungana na Rais Samia katika kuhamaisha wananchi kutumia nishati hiyo.Ahadi yetu kwa Serikali tutaendelea kuhamasisha kwa kugawa bure mitungi na majiko kwa makundi mbalinbali ya wananchi.

Akieleza zaidi amesema kutumia nishati safi ya kupikia kunafaida kubwa za kiafya na kimazingira lakini wakati huo huo inatoa nafasi kubwa ya watoto kupata nafasi ya kwenda shule kupata elimu badala ya kutumia muda mwingi kwenda kukusanya kuni.

”Nakushukuru Waziri Mchengerwa kwa kufanikisha mpango huu wa nishati safi ya kupikia kwa wnanchi wa Rufiji kwa kuwapatia mitungi ya gesi 900."

Awali Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Pwani, Jenipher Shirima ameeleza kwa kina namna ambavyo vimetungi ya gesi inaweza kutumika kwa usalama bila kuleta athari.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania( wa tatu kushoto) akikimkabidhi mtungi wa gesi ya Oryx na jiko lake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania(UWT) Marry Chatanda(wa pili kulia) na Mbunge wa Jimbo la Rufiji ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa( wa tatu kulia).Mitungi hiyo imekabidhiwa kwa Mwenyekiti  wa UWT kabla ya kuanza kuigawa kwa Mama Lishe wote wa Wilaya ya Rufiji ambapo jumla ya mitungi 900 ya gesi ya Oryx na majiko yake imekabidhiwa kwa mamalishe.Wengine wanaoshuhudia ni Katibu Mkuu UWT Jokate Mwegelo( kushoto) , Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Wanu Hafidh Ameir( wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Zainab Vullu( kulia)
Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman ( katikati) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania( UWT) Marry Chatanda( wa pili kulia),  Katibu Mkuu wa UWT Jokate Mwegelo(wa tatu kulia) , Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa(wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa Oryx na jiko lake mmoja wa Mama Lishe wa Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani( wa tatu kushoto), lengo ni kuwawezesha Mama Lishe kutumia nishati safi ya kupikia badala ya kuni na mkaa.Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja Masoko wa Oryx Peter Ndomba na kulia ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa Pwani Zainab Vullu.Jumla ya mitungi 900 ya Oryx Gas na majiko yake yametolewa bure kwa Mama Lishe wote wa Wilaya hiyo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad