HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 12, 2023

BASHE ATAKA UCHUNGUZI UFANYIKE KUBAINI HUJUMA KATIKA MKONGE HUKU AKIFUTA LESENI KWA JABARI INVESTMENT KAMPUNI YA KOROSHO.

 
Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ameelekeza kamati ya ulinzi na usalama inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Waziri Kindamba kuchunguza kwa kina ili kubaini kampuni ilisafirisha nyuzi za mkonge zilizochanganyika na uchafu. Mheshimiwa Bashe amekiita kitendo hicho ni cha uhujumu uchumi na usaliti kwa zao la Mkonge akiwa katika mkutano wa Mwaka wa nne wa wadau wa zao la mkonge kilichochafanyika Korogwe Tanga leo Tarehe 12 Desemba 2023.

Malengo ya vitendo kama hivi ni kutaka kudhoofisha masoko na juhudi za serikali ya awamu ya sita na kurudisha nyuma jitihada la kufufua zao hilo na hivyo atakae bainika kuhusika achukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine alisisitiza Mheshimiwa Bashe.

Aidha Mheshimiwa waziri wa kilimo amemuelekeza Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Korosho kuifutia leseni kampuni ya JABARI INVESTMENT iliyopewa nafuu za kikodi na nyinginezo za kununua na kubangua Korosho ghafi toka kwa wakulima lakini cha kustaajabisha kampuni hio inatumia vifungashio vinavyotambulisha korosho hio imezalishwa Vietnam.

Bashe amesema kampuni ya JABARI INVESTMENT kwa makusudi inahujumu zao la korosho na jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani serikali imegharimia zaidi ya billioni 100 za ruzuku ili kuongeza na kukuza tija katika zao hilo.

Amezionya kampuni za namna hii kuacha mara moja michezo ya namna hii kwani serikali ya awamu ya sita haiko tayari kufumbia macho aina yoyote ya hujuma katika sekta ya kilimo. Kesho Mheshimiwa Bashe ataendele na ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad