HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 22, 2023

WAZIRI MKUU MGENI RASMI MATEMBEZI YA MARIDHIANO NA AMANI

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania, Shekhe Alhaji Musa Salum akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Novemba 22, 2023 wakati wa kutambulisha matembezi ya Maridhiano na Amani Tanzania yatakayofanyika Desemba 2, 2023 jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Richard Hananja akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Novemba 22, 2023 wakati wa kutambulisha matembezi ya Maridhiano na Amani Tanzania yatakayofanyika Desemba 2, 2023 jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano na Amani, Mchungaji Samweli Akanyugikaakabonaki akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Novemba 22, 2023 wakati wa kutambulisha matembezi ya Maridhiano na Amani Tanzania yatakayofanyika Desemba 2, 2023 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza Jumuiya ya Maridhiano na Amani jijini Dar es Salaam leo Novemba 22, 2023.

WAZIR Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika matembezi ya Maridhiano na Amani ya Mama Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yatakayofanyika kuanzia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam Desemba 02, 2023.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Novemba 22, 2023, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania, Shekhe Alhaji Musa Salum amesema Matembezi hayo yatakuwa kuanzia Kilomita 2, 5, 10 na 21 na yataanzia katika viwanja vya Karimjee kuelekea Barabara ya Aghakhan, Daraja la Tanzanite mpaka Seeclif hoteli.

"Nathibitisha kushiriki pamoja na kumuunga Mkono Mama yetu Samia Suluhu Hasan, na tayari nishanunua tiketi yangu, nawe nunua tiketi yako pia." Amesema

Akizungumzia Mahali zinakopatikana tiketi hizo, Shekhe Alhaji Musa Salum amesema tiketi zinapatikana katika ofisi ya Maridhiano na Amani Tanzania, Mlimani City pamoja na City Gurden.

Pia amewakaribisha watanzania wote kushiriki matembezi ya amani na Mama Dkt. Samia Suluhu Hassan na kumuunga mkono kwa matendo.

Kwa Upande wa Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano na Amani, Mchungaji Samweli Akanyugikaakabonaki amewaomba watanzania kujumuika pamoja nao katika Matembezi hayo kwa kuchagua ni Kilomita ngapi unataka kutembea.

Akithibitisha kushiriki Matembezi hayo, Mchungaji Richard Hananja amesema kuwa amani ni kitu adimu sana duniani, pasipo amani hakuna chochote kinachoweza kuendelea, hivyo ameiomba jamii kwa ujumla kununua tiketi ili waweze kudumiasha amani iliyopo nchini na kuunga na mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kudumisha amani iliyopo ili izidi kudumishwa kwa Matendo.

"Hatuhitaji Upendo wa Maneno, Walaka wa kwanza 1 Yohana 3:18 Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli. Upendo ni Matendo, Mungu atubariki tufikie siku hiyo kwa Mapenzi ya Mungu, matendo yetu yataonesha upendo wa kweli kama sisi Watanzania tumeridhiana, tunakaa kwa amani huo ndio Utu." Amemalizia kwa Kuwabariki

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad