Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kwa kushirikiana na Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya(ECAC) kimeendesha kozi ya kuwajengea Uwezo wa Kiukaguzi ya siku tano kwa wakaguzi wa Usafiri wa Anga 10 kutoka nchini Tanzania na Somalia.
Akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari, Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usalama wa Usafiri wa Anga Thadeo Nondoli amewataka washiriki wa kozi hiyo kwenda na kufundisha wengine walichojifunza kwa manufaa ya jumuiya nzima ya usafiri wa anga na sio kujinufaisha peke yao.
Bw. Nondoli aliwashukuru washiriki hao wa kozi hiyo kwa kuichagua CATC ambayo pia ni moja katika vyuo vya mafunzo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga(ASTC) kuwa sehemu ya kufanyia mafunzo yao hayo.
Kozi hiyo ilyodhaminiwa na Umoja wa Ulaya (EU), ilikuwa ya nadharia na vitendo katika uwanja wa ndege ambapo washiriki kutoka TCAA, Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA)upande wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA), Dar es Salaam na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Kilimanjaro, Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar(ZAA) na wengine watano kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Somalia(SCAA) walitembelea JNIA.
Awali, akimkaribisha Mgeni rasmi Mkuu wa Chuo CATC Aristid Kanje ili kufunga mafunzo hayo yaliyoanza Novemba 13-17, 2023, alisema CATC hivi sasa ipo katika mchakato wa kujenga chuo cha kisasa cha Usafiri wa Anga na kuwakaribisha washiriki kurudi tena CATC kwa mafunzo zaidi.
Kanje alisema CATC lengo lake ni kuhakikisha wanachuo wanafikia viwango vya juu vya ufaulu na mafanikio katika masuala ya usafiri wa anga na kuongeza kuwa CATC sio tu inatoa mafunzo ya ratiba bali hata kuandaa mafunzo maalum kwa kukidhi mahitaji wa waombaji.
Awali Mkufunzi kutoka ECAC Charlote Lund aliishukuru CATC kwa kuratibu mafunzo hayo kwa ufanisi katika kipindi chote cha mafunzo na kuwapongeza washiriki wa kozi kwa kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu licha kuwa wametoka mataifa tofauti.
Kozi hiyo ya siku tano kwa upande wa CATC ilisimamiwa na John Richard Ndimbo ambaye ni Mkufunzi Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Usafiri wa Anga CATC.
Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usalama wa Usafiri wa Anga Thadeo Nondoli akizungumza wakati wa kufunga kozi ya kuwajengea Uwezo wa Kiukaguzi ya siku tano kwa wakaguzi wa Usafiri wa Anga 10 kutoka nchini Tanzania na Somalia iliyofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kwa kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa kushirikiana na Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya(ECAC).
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akizungumza kuhusu kazi zinazofanywa na chuo hicho wakati wa kufunga kozi ya kuwajengea Uwezo wa Kiukaguzi ya siku tano kwa wakaguzi wa Usafiri wa Anga 10 kutoka nchini Tanzania na Somalia iliyofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kwa kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa kushirikiana na Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya(ECAC).
Mkufunzi kutoka ECAC Charlote Lund akizungumzia mchango wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa kushirikiana na Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya(ECAC) na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) walivyoweza kuedesha kozi ya kuwajengea Uwezo wa Kiukaguzi ya siku tano kwa wakaguzi wa Usafiri wa Anga 10 kutoka nchini Tanzania na Somalia.
Mkufunzi Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Usafiri wa Anga CATC, John Richard Ndimbo akizungumza kuhusu mafunzo yalivyofanyika wakati wa kufunga kozi ya kuwajengea Uwezo wa Kiukaguzi ya siku tano kwa wakaguzi wa Usafiri wa Anga 10 kutoka nchini Tanzania na Somalia iliyofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kwa kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa kushirikiana na Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya(ECAC).
Abdi Rahman Mohammed kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Somalia (SCAA) akitoa shukrani kwa Umoja wa Ulaya (EU) kwa kushirikiana na Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya(ECAC) kwa kuwapa mafunzo yaliyofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usalama wa Usafiri wa Anga Thadeo Nondoli (wa pili kushoto) akitoa vyeti kwa washiriki wa kozi ya kuwajengea Uwezo wa Kiukaguzi ya siku tano kwa wakaguzi wa Usafiri wa Anga 10 kutoka nchini Tanzania na Somalia iliyofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kwa karatibiwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa kushirikiana na Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya(ECAC).
Baadhi ya wakaguzi wa Usafiri wa Anga 10 kutoka nchini Tanzania na Somalia, wakufunzi kutoka Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya (ECAC) wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usalama wa Usafiri wa Anga Thadeo Nondoli aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari.
Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usalama wa Usafiri wa Anga Thadeo Nondoli akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), wakufunzi kutoka Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya (ECAC) na wakaguzi wa Usafiri wa Anga 10 kutoka nchini Tanzania na Somalia mara baada ya kufunga Kozi ya kuwajengea Uwezo wa Kiukaguzi iliyofanyika kwa siku tano.
No comments:
Post a Comment