HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 11, 2023

Waziri Jenister Mhagama akoshwa na mshiko fasta ya NMB

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Baraka Ladislaus (kulia) akimuelezea juu ya huduma za taasisi hiyo kwenye maadhimisho ya wiki ya Vijana Kitaifa iliyoanza Oktoba 8, 2023 na kutarajia kumalizika Oktoba 14, 2023 katika Viwanja vya Babati mkoani Manyara.

Na Cathbert Kajuna - MMG/Kajunason, Manyara.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amewataka vijana kuchangamkia fursa ya mkopo fasta inayotolewa na benki ya NMB katika kujikwamua kiuchumi.

Hayo ameyasema Waziri Mhagama mkoani Manyara kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya Vijana Kitaifa yaliyoanza Oktoba 8 na yatafikia tamati Oktoba 14, 2023 wilayani Babati mkoani Manyara.

Mhagama amesema kuwa mkopo wa mshiko fasta inayotolewa na benki ya NMB, umejipambanua katika malengo makubwa ya maadhimisho hayo ambayo ni kutatua changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo ukosefu wa mitaji na ajira.

"Nimependa hiyo huduma ya mshiko fasta naomba vijana wachangamkie hiyo fursa na ninyi viongozi wahamasisheni wananchi kuzitumia katika kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi"

Awali, Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Baraka Ladislaus (kulia) amesema wamefikia kubuni huduma hiyo ya mkopo waliyoiita 'mshiko fasta' kwa ajili ya kuwarahisishia wateja wao wanaofanya shughuli za kiujasiriamali kupata fedha za haraka kupitia simu zao za mkononi.

"Huduma hii unalenga kuwasaidia wajasiriamali kupata mkopo wa haraka kupitia simu zao za mkononi kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kila siku"

Amesema kuwa mteja anaweza kukopa Hadi kiasi cha shilingi 500,000 bila kufika katika tawi la Benki na wala kuweka dhamana yeyote.

Mmoja wa wajasiriamali katika maonyesho hayo, Eva Martine amesema kuwa mkopo huo wa NMB unawaokoa na fedha zenye masharti magumu zinazotolewa na watu mitaani.

"Huu mkopo wa NMB, umekuja wakati muafaka kutuepisha na kausha dam, kwani Mimi ambae napika hapa stendi siku nikiamka nimetumia hela yote kwa matumizi mengine nakopa hela huko nakwenda kununua mahitaji ya kupika na biashara inaendelea huku nikifanya marejesho" alisema Eva.

Lengo la maadhimisho hayo ni kuwawezesha vijana kupata jukwaa la kujadili fursa zinazozotolewa na serikali na kutatua changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo ukosefu wa mitaji na ajira. 

Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa 2023 yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu yakiwa na kauli mbiu, "Vijana na Ujuzi Rafiki wa Mazingira kwa Maendeleo Endelevu"

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad