HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 21, 2023

MAHAFALI YA 12 YA PSPTB YAFANA, SERIKALI YATOA MAELEKEZO KWA WAHITIMU KUHUSU MAADILI YA KAZI

 


Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya Ununuzi na Ugavi, wameaswa kuzingatia maadili na weledi katika majukumu yao.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Jenifa Omolo katika mahafali ya 12 ya Wahitimu 269 wa Mitihani ya Kitaaluma ya Ununuzi na Ugavi yalifanyika leo Oktoba 21, jijini hapa.

Omolo amewata kusimamia viapo vyao kwani suala la maadili na weledi ni changamoto hususani katika sekta hiyo ya ununuzi na ugavi kwa muda mrefu.

Aidha ameongeza kuwa ili kuendelea kuongeza ununuzi na ugavi bodi hiyo inapaswa kuongeza thamani ya programu zao ikiwa ni pamoja na kuongeza fursa za mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi ili kuwajengea uwezo wa kujiajiri.

"Sisi kama wizara tutashirikiana nanyi katika kufanya mabadiliko chanya ya kuongeza thamani ya taaluma ili iweze kuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa," amesema Omolo.

Vilevile ameielekeza Bodi ya Wataalamu wa Mitihani ya Kitaaluma ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kuchukua hatua zaidi ili kuimarisha usimamizi wa fani hiyo hususani katika kusimamia mitaala ya vyuo kwa lengo la kukuza weledi na maadili ya wahitimu.

Akizungumzia mtaala mpya uliozinduliwa katika mahafali hayo ambao unahusisha masomo mahususi ya maadili ya kitaaluma, Usimamizi wa mkataba, mali, ujuzi na ushauri elekezi kitaalamu na masuala ya kiongozi, Omolo amesema:

"Ninaipongeza bodi kwa kuandaa mtaala huu ambao utasaidia katika kutekelezeka mkakati wa Serikali wa kutekeleza ununuzi wa kimkakati," amesema Omolo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Jacob Kibona amezitaja changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika kada hiyo.

Amesema kuna waajiri ambao wanaajiri wataalamu ambao hawajasajiliwa ambao hawatambuliki kisheria jambo ambalo linasabisha kushindwa kuwachukulia hatua za kinidhamu pale wanapokiuka taratibu za kimanunuzi.

"Kuna uwepo wa Wadau mbalimbali wanaoingilia michakato ya ununuzi na ugavi hivyo kusababisha usumbufu Kwa Wataalamu walisajiliwa na kushindwa kufanya majukumu yao," amesema Kibona.

Kibona ameongoza kuwa kuporomoka kwa maadili katika jamii ni changamoto nyingine kwani wataalamu hao Wako Katikati ya jamii jambo ambalo ni rahisi kuathiri uadilifu wa wataalamu wa kada hiyo.

Naye mhitimu wa kozi ya Ununuzi na Ugavi kupitia mitihani ya kitaaluma ya PSPTB, Ester Mshana amesema licha ya changamoto ya ajira anaweza kutumia ujuzi alioupata kujiajiri.

"Kupitia elimu hii, tunafahamu ni vitu gani vya kufanya tunapoingia mtaani. Hata kama hakuna ajira Serikalini, masomo ya ujasiriamali tuliyosoma yanatupa uwezo wa kujiajiri," amesema Ester.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Jenifa Omolo (kushoto) akizindua mtaala mpya wa Masomo ya Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakati wa Mahafali ya 12 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB. Katikati ni Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Jacob Kibona na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godfred Mbanyi 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Jenifa Omolo (kushoto)  akionesha mtaala mpya wa Masomo ya Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) uliozinduliwa wakati wa Mahafali ya 12 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB. Katikati ni Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Jacob Kibona na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godfred Mbanyi 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Jenifa Omolo akizungumza wakati wa Mahafali ya 12 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB ambapo amewaasa yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu mkuu alimwakilisha Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Natu E. Mwamba.

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Jacob Kibona akizungumza katika Mahafali ya 12 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB  kuanzishwa kwa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi 2007 nakusema kuwa kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha bodi matokeo yote ya mitihani ya bodi ni lazima yapitiwe na kuidhinishwa na bodi ya Wakurugenzi.

Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godfred Mbanyi akizungumza wakati wa Mahafali ya 12 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB ambapo amewaasa wahitimu kufanya kazi kwa kufata maadili ya kitaaluma ili kulinda heshima ya fani yao na kuleta ufanisi katika matumizi ya rasirimali za umma kwa manufaa ya Taifa wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Mshehereshaji ambaye ni Meneja Masoko na Uhusiano Kwa Umma (PSPTB)Bi Shamim Mdee akizungumza jambo wakati wa Mahafali ya 12 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Jenifa Omolo akitoa zawadi kwa baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani ya Bodi wakati wa mahafali ya 12 ya Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Jenifa Omolo akiwatunuku wahitimu wa walioudhuria Mahafali ya 12 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa kitengo cha Sheria PSPTB Piencia Kiure akiwaapisha Wahitimu wa mahafali ya 12 ya Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kiapo cha kiapo cha utii, uadilifu na uaminifu
Wahitimu wa mahafali ya 12 ya Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakila kiapo cha utii na uaminifu 
Baadhi ya Wageni waalikwa pamoja na wafanyakazi wa PSPTB wakifuatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Jenifa Omolo wakati wa Mahafali ya 12 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB.
Baadhi ya wahitimu wakifuatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Jenifa Omolo wakati wa Mahafali ya 12 ya Wahitimu wa Mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Picha mbalimbali za pamoja katika mahafali ya 12 ya  wahitimu wa mitihani ya kitaaluma ya PSPTB

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad