HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 12, 2023

LUOGA AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO KITAIFA JUMA LA ELIMU YA WATU WAZIMA

 

Mgeni rasmi  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Msingi kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia  Josephat Luoga akiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya washiriki  katika kongamano  hilo la maadhimisho  ya  kitaifa ya juma la elimu  ya watu wazima.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu ya Msingi kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Josephat Luoga

Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
KAIMU Mkurugenzi Idara ya Elimu Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Josephat Damas Luoga leo Oktoba 12 ,2023 amezindua

Kongamano la maadhimisho ya Kitaifa ya Juma la Elimu ya Watu Wazima lenye Kauli Mbiu isemayo kukuza uwezo wa kusoma na Kuandika kwa Ulimwengu unaobadilika kujenga misingi ya jamii endelevu na nyenye amani.

Luoga amesema kuwa mwaka 1961 baada ya nchi ya Tanganyika kupata Uhuru wake kutoka kwa mkoloni, aliyekuwa Rais wa Kwanza Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitoa mafunzo ya elimu ya watu wazima kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumia vipindi mbalimbali vya redio, magazeti, mikutano jambo ambalo kwa wakati huo asilimia 80 watu walikua hawajui kusoma na kuandika lakini ilipofika mwaka 1986 idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika ilipungua na kufika asilimia 9.6.

Uzinduzi huo umefanyika leo kwenye Ukumbi wa wauguzi uliopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

Afisa Elimu Mkoa wa Pwani Bi. Sara Mlaki ametoa salamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kuwa mkoa huo unajivunia kwa kuwa kwa kupitia kongamano hilo umefaulu kwa asilimia 99 kupitia utoaji wa elimu ya Memkwa na njia zingine za utoaji wa elimu huku mpango wa memkwa kwa watoto waliokuwa darasa la nne wamefaulu wote kwa asilimia 99 na kuweza kuendelea na elimu ya Shule za Msingi za kawaida.

"Mafanikio haya ni nyenzo kuu katika kukuza uchumi wa viwanda ndani ya Mkoa wetu na ni jambo la kushukuru kwa ujumla kwa kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa kilele huku yakiwa tayari yameshafanyika katika Mikoa mbalimbali nchini." Amesema Bi Mlaki.

Mtoa mada pia mshiriki Maggid Mjengwa amesema kuwa jamii ianze kuidadavua elimu ya watu wazima kwa kuwa siyo mahsusi kwa wazee na vikongwe na kwamba mtu yeyote anayesoma iwe kwa kwenda maktaba au kwa njia ya mtandao hizo zote ni elimu za watu wazima kwani sifa za kibailojia katika kumtambukisha mtu mzima ni yule mwenye umri kati ya miaka 35 hadi 60 na kwamba hii ni elimu huru kwa kila aliyekosa nafasi ya kupata elimu.

Mwasilishaji Paulina Mkoma amesema kuwa wadau wa Halmashauri wanapaswa waweke utaratibu wa kutembelea vituo vinavyotoa elimu hizo licha ya kuwa kuna changamoto mbalimbali ya namna ya kufika kwenye vituo hivyo ili waweze kuwakangua na kuwapa miongozo.

"Elimu hii ya Watu wazima itaingizwa kwenye maboresho ili iweze kutolewa kwa watu wote bila kuangalia umri.

Washiriki wa kongamano hilo wametoka katika Mikoa mbalimbali nchini huku watoa mada wake ni pamoja na Dkt. Blackson Kanukisya, Paulina Mkoma, Dkt. Mpoki Mwaikokesya, Frauke Heinze, Hinju Kimweri, Maggid Mjengwa, Dkt. Sempeho Siafu, Dkt. Margareth Matonya pamoja na Dkt. Philipo Sanga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad