Na Mwandishi wetu
MKUU wa Mkoa wa Geita Martin Shigella ameishauri kampuni ya Al mansour Tanzania ambao ni wauzaji na wasambazaji wa magari aina ya ISUZU kuchangamkia fursa zinazopatikana kanda ya Ziwa.
Fursa hizo ni katika sekta ya madini kwa kushiriki maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa za madini yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni katika mkoani humo.
Akizungumza jijjini Dar salaam hivi karibuni alipotembelea ofisi ya Kampuni ya ISUZU, Shigella amesema ni muhimu kampuni ya Al mansour Tanzania kuchangamkia fursa lukuki zinazopatikana kanda ya Ziwa kwa sasa.
"Niwaombe Al mansour Tanzania muanza kuchangamkia fursa zinazopatikana ndani ya Mkoa wa Geita,mojawapo kubwa ni hii ya kushiriki maonesho ya Kimataifa ya bidhaa za madini yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni '',amesema Shigella.
Ameongeza lengo la kuwahamasisha ushiriki wa maonesho hayo,ni kuona na wao wanaitumia fursa hiyo kutanua wigo wa biashara zao,kukutana na wafanyabiashara wapya ikiwemo na hata kubadilishana mawazo katika suala zima la uwekezaji katika maeneo mbalimbali .
Amesema kwa kufanya hivyo pia watakutana na wadau walioko katika sekta za madini ukanda huu wa Afrika Mashariki,wakiwa na bidhaa/magari yao kuyatangaza zaidi na kuwa na soko la uhakika kanda ya ziwa.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa kampuni hiyo nchini Tanzania Anurup Chatterjee amesema ni faraja kwao kutembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, wao wanathamini jitihada zilizowekwa na serikali kuhakikisha maonesho yanafanikiwa na kuleta tija.
"Sisi kama kampuni ya Magari ya ISUZU tunawahakikishia wateja wa Kanda ya Ziwa wasipate usumbufu, tumedhamiria kushiriki maonyesho hayo ukizingatia mwaliko alioutoa Mkuu wa Mkoa,kwetu sisi ni maagizo hivyo hatutomwangusha'',amesema Chatterjee
Amesisitiza atahakikisha timu mzima ya mauzo inaweka kambi kanda ya ziwa kwa kipindi chote


.jpeg)

No comments:
Post a Comment