TCAA YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAHARUKI KUHUSIANA NA AJALI YA NDEGE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 26, 2023

TCAA YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAHARUKI KUHUSIANA NA AJALI YA NDEGE

 

Kufuatia taharuki ya kuanguka kwa ndege maeneo ya Mkuranga Mkoani Pwani, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imewatoa hofu wananchi kuhusiana na tukio hilo na kwamba hilo lilikuwa ni zoezi la kutathmini utayari pindi linapotokea ajali katika usafiri wa anga hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Flora Alphonce amesema zoezi hili limehusisha vyombo mbalimbali vya uokoaji ambavyo ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Zimamoto, Shirika la Msalaba Mwekundu, TANAPA , TASAC, Jeshi la Polisi nk. ili kujiweka tayari kipindi wanapopata ajali halisi katika anga la Tanzania.

Amesema zoezi hili litafuatiwa na tathmini ya pamoja kutoka kwa wataalamu walioshiriki zoezi hilo na TCAA itatoa taarifa kamili  kwa vyombo vya habari kesho tarehe 27 Julai, 2023.

Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Alphonce (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutokea kwa taharuki kwa wananchi wakati wa zoezi la uhokoaji lenye lengo la kupima ufanisi katika taasisi mbalimbali zinazotoa huduma katika maeneo mbalimbali ya Usafiri wa anga. Kulia ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw Yessaya Mwakifulefule
Meneja Mahusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw Yessaya Mwakifulefule (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uhokoaji lenye lengo la kupima ufanisi katika taasisi mbalimbali zinazotoa huduma katika maeneo mbalimbali ya Usafiri wa anga. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Alphonce.
Mkutano ukiendelea 

Picha za Chini ni wakati wa zoezi


Vikosi vya ulinzi na usalama vikiendelea na zoezi la uhokoaji 
Muonekano wa mfano wa ndege iliyokuwa inatumika kwenye 
zoezi la kutathmini utayari pindi linapotokea ajali katika usafiri wa anga

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad