WATUMISHI WA TCAA WAHIMIZWA KUENDELEA KUCHAPA KAZI KWA USHIRIKIANO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 28, 2023

WATUMISHI WA TCAA WAHIMIZWA KUENDELEA KUCHAPA KAZI KWA USHIRIKIANO

  Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wamehimizwa kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuendelea kutenda kazi kwa ufanisi.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi Mrope amewataka wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la TCAA lililofanyika Aprili 28,2023 mjini Morogoro.

"Tunatambua umuhimu wa TCAA katika maendeleo ya nchi yetu lakini TCAA inajengwa kuianzia na wewe mtumishi mmoja, nawasihi sana mfanye kazi kwa kushirikiana kila mmoja kwa nafasi yake na inapobidi msaidie mwingine ili kuhakikisha malengo ya taasisi na serikali kwa ujumla yanafikiwa na huduma inatolewa" amesema Bw.Mrope

Awali akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza S. Johari amesema Mamlaka inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ukiwemo wa kuboresha Mfumo wa Masafa ya Mawasiliano wa Sauti baina ya rubani na waongozaji ndege katika vituo vyote vya kuongozea ndege nchini.

Baraza hilo limefanyika kwa siku moja ambapo mbali na kujadili masuala kadhaa yanayoihusu TCAA wajumbe wamepata nafasi ya kupiga kura na kumchagua mfanyakazi bora wa Mamlaka kwa mwaka huu wa fedha.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi Mrope akibonyeza kitufe kama ishara ya uzinduzi wa kitabu kinachoonesha maboresho na mageuzi makubwa yaliyofanyika ndani ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA). Bw. Mrope alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la TCAA lililofanyika Aprili 28,2023 mjini Morogoro
Mgeni rasmi na meza kuu wakitazama picha jongefu zikionesha uzinduzi wa kitabu kinachoonesha maboresho na mageuzi makubwa yaliyofanyika ndani ya TCAA.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi Mrope akizungumza wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la TCAA lililofanyika Aprili 28,2023 mjini Morogoro.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la TCAA lililofanyika Aprili 28,2023 mjini Morogoro.
Watumishi wa TCAA wakifuatilia shughuli za ufunguzi wa Baraza.
Wajumbe wa Baraza wakiimba wimbo wa mshikamano
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari akimkabidhi Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi Mrope kitabu kinachoonesha maboresho na mageuzi makubwa yaliyofanyika ndani ya TCAA.
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la TCAA Bw. Mweya Didacus akizungumza wakati wa mkutano huo
Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad