HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 21, 2023

TASAC yatoa mafunzo Kukabiliana na Umwagikaji wa Mafuta Baharini

 


*Yaahidi kuendelea kutoa mafunzo kutokana na mahitaji yanayobadilika kila wakati.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV.
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limekutana na wadau mbalimbali wa mkoa Dar Es Salaam na Pwani katika kutoa elimu ya Mpango wa Taifa wa kukabiliana na umwagikaji wa mafuta baharini.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Mha.Selestine Mkenda ambaye Kaimu Meneja usalama na utunzaji wa Mazingira alisema "TASAC imeona umuhimu wa kutoa uelewa ya kuweza kukabiliana na umwagikaji wa mafuta na kuchukua hatua za awali kuzuia madhara kwa viumbe hai vya bahari na shughuli za uchumi."

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau na TASAC uliofanyika Mjini Bagamoyo Mkuu Wilaya ya Bagamoyo Halima Habibu amesema kuwa "mafuta yakimwagika unaathiri uchumi wa nchi."

Amesema " Shughuli kubwa ya Uchumi Bagamoyo ni Uvuvi, hivyo elimu ya TASAC imekuja sehemu sahihi juu ya Mpango wa Taifa kukabiliana na umwagikaji wa mafuta baharini.

Amesema kuwa hata yeye atakuwa Balozi wa kuzungumza juu ya uelewa wakati atapokuwa ameshiriki mafunzo yatayotolewa na wataalam kwa vitendo.

Amesema suala la umwagikaji wa mafuta lazima lijadiliwe kwa wadau wote kwani Bahari ndio maendeleo kwa mwananchi wa mkoa wa Pwani. Hivyo, hatua zote zitumike katika majanga kama hayo yakitokea hatua zichukuliwe haraka.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Kaimu Abdi Mkeyenge , Meneja wa Usalama wa Meli , Ulinzi na Mazingira Selestine Mkenda katika mkutano huo wadau walioshiriki watakuwa ndio watoa taarifa wakati mafuta yamemwagika.

Amesema kuwa mafuta yakimwagika katika bahari ni janga ambapo meli husika inatakiwa kulipa fidia kuhusiana na uchafuzi wa mazingira katika bahari.

Amesema kuwa uwepo wa wadau wenye mafunzo na uelewe watakuwa wanajua wanachukua hatua gani pale mafuta yanapokuwa yanamwagika.

Mkenda amesema kuwa "wadau kama Wavuvi wakiwa na uelewa kwani wao ndio watu wa kwanza kwenye bahari wakiona mafuta watajua wanafanya nini kukabiliana na umwagikaji wa mafuta hayo.

Amesema kuwa mafuta yakimwagika kazi kubwa ni kusafishwa katika kulinda mazingira pamoja na viumbe hai majini".

Mdau wa Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu Claver Mwaikambo amesema kuwa "majanga hayo yameshatokea sehemu mbalimbali na kuleta madhara makubwa.

Amesema kuwa wakati wa suala ya kukabili lazima kuangalia afya na usalama wa mazingira ya mafuta yaliyomwagika.

Mwaikambo amesema kuwa umwagikaji wa mafuta kazi kubwa kwani kunahitaji kuwa na sheria za ndani nje ya sheria ya mkataba.

Mmoja ya Mvuvi Salum Ahmad amesema kuwa elimu ya umwagikaji wa mafuta baharini kwao imefika wakati mwafaka kwani wao ndo watu wa kwanza pindi likitokea meli kumwaga mafuta.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Halima Habibu akiwa katika picha ya pamoja na wadau walioshiriki mafunzo ya Kukabiliana na Umwagikaji wa Mafuta Baharini Mjini Bagamoyo.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Halima Habibu  akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abbakari Kunenge wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mafunzo kwa Wadau namna ya kakabiliana na majanga ya umwagikaji wa mafuta baharini, Mjini Bagamoyo
Meneja wa Usafiri wa Meli , Ulinzi na Mazingira wa TASAC Selestine Mkenda kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAC  Kaimu Abdi Mkeyenge  akitoa maelezo kuhusiana na wadau kuhusu mafunzo ya kuweza kukabiliana na umwagikaji wa mafuta baharini, Mjini Bagamoyo.
Mdau wa Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu Claver Mwaikambo akizungumza na waandishi wa wadau kuhusiana namna ya kukabiliana na umwagikaji wa mafuta na  jinsi ya kutoa mafuta hayo kwenye mkutano wadau hao uliofanyika Mjini Bagamoyo.
Katibu wa Chama cha Wavuvi Bagamoyo Salum Ahmad akizungumza kuhusiana na mafunzo ya Umwagikaji wa mafuta baharini wakati imetokea namna ya kuweza kutoa taarifa, mjini Bagamoyo.
Meneja Afya , Usalama , Ulinzi , Mazingira na ubora mahala pa Kazi kutoka TIPER    Leah John Wandwi  akizungumza akiwasilisha kazi ya kikundi kazi kwenye mafunzo ya wadau namna ya kukabiliana na umwagikaji mafuta Baharini Mjini Bagamoyo.
Wadau na wakiwa katika mafunzo yaliyoratibiwa na TASAC kwa ajili ya kiwajengea uwezo namna ya kukabiliana na umwagikaji wa mafuta baharini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad