HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 22, 2022

Agricom Yasisitiza Watanzania Kutumia Zana za Kisasa za Kilimo, Yatuma Salaam za Krismass na Mwaka Mpya

 WATANZANIA wamehimizwa kutumia zana bora na za kisasa za kilimo kwa kuchangamkia fursa za kilimo biashara, ili kuzalisha bidhaa nyingi za kilimo zitakazo tumika kama malighafi ya viwanda, hivyo makampuni ya zana za kisasa na pembejeo za kilimo kama Agricom Africa Limited, zimepongezwa kwa kazi nzuri, na serikali kuahidi kuzipa kila aina ya ushirikiano ili kufanikisha Agenda 1030 ya kilimo biashara.


Pongezi hizo, zimetolewa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dr. Ashatu Kijaji, kwenye mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii, mara baada ya kuhudhuria hafla ya Siku ya Sekta Binafsi nchini, TPSF, iliyofanyika Masaki jijini Dar es Salaam, hivi karibuni ambapo Kampuni ya Agricom Africa Limited ilipata tuzo, na kukabidhiwa tuzo hiyo na Makamo wa Rais, Dr. Isdore Mpango, aliyekuwa mgeni rasmi.

Dr. Kijaji amesema, kwa kutambua umuhimu wa sekta binafsi ndio injini ya uchumi wa taifa, serikali imeongeza bajeti ya kilimo kutoka bilioni 254 mpaka bilioni 964, ili kufanya uwekezaji kwenye kilimo kuelekea kilimo biashara ili kuzalisha malighafi ya kutosha kukidhi mahitaji ya Tanzania ya Viwanda, hivyo wazalishaji wa zana bora na za kisasa za kilimo, watawezeshesha agenda ya 1030 ya kilimo biashara kufanikiwa na sekta ya kilimo kuwa mzalishaji mkuu wa malighafi ya viwanda.

Pia Waziri Kijaji, amesema serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dr. Samia Suluhu, inatambua sekta binafsi injini ya ukuaji wa uchumi wa taifa, ndio maana imeweka kipaumbele muhimu kwa kuishirikisha sekta binafsi kwa kuboresha zaidi mazingira ya biashara, ndio maana rais Samia, akisafiri nje, anaandamana na sekta binafsi, sekta binafsi ikifanikiwa ni Tanzania imefanikiwa.

Kwa kuanzia serikali imebadili sheria ya Uwekezaji na kuwajumuisha wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa kwa kuwatambua kama wawekezaji, hivyo kufaidi vivutio vya uwekezaji, pia serikali imeishafuta tozo na ushuru sumbufu zaidi ya 230 kwenye serikali kuu, sasa serikali inakwenda kuziangazia tozo sumbufu kwenye serikali ili nazo izifute na kuboresha zaidi mazingira ya kufanya biashara.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Agricom Africa Limited, Alex Duffar, katika salaam zake za Krisimasi na Mwaka mpya, amezungumzia mafanikio makubwa ya kampuni ya Agricom, ndie msambazaji mkuu wa zana za kisasa za kilimo, ambapo kwa mwaka jana waliuza matrekta 1,400, lakini mwaka huu wameisha uza zaidi ya matrekta zaidi ya laki moja.

Bwana Duffar, amesema Agricom Africa Limited, wameidhamini Taasisi ya Sekta Binafsi nchini TPSF, kwasababu Agricom wao ni daraja na kufikia mafanikio ya kilimo kwanza na Agenda 1030 ya kilimo Biashara.

Afisa Masoko wa Agricom Africa, Baraka Konkara, amesema Agricom wanajivunia kuwa wasambazaji wakubwa wa zana za kisasa za kilimo, hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kuendeleza sekta ya kilimo, haswa kwa kuzingatia, asilimia 70 ya Watanzania, wanategemea kilimo.


Makamu wa Rais, Dk. Philip Isidor Mpango (kushoto), akikabidhi tuzo kwa Alex Duffar, ambaye ni Group CEO wa kampuni ya Bravo Group, kampuni mama wa Agricom Africa, wakati wa hafla ya siku ya Sekta Binafsi nchini, TPSF Day. Kulia ni Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula. Nyuma ni na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Awali kwenye maadhimisho ya siku ya sekta binafsi nchini, TPSF, Mwenyekiti wa TPSF, Bi. Angelina Ngalula, alimtunuku zawadi maalum rais Samia kwa juhudi za serikali yake kuboresha Mazingira ya biashara, zawadi iliyopokelewa na Makamo wa Rais aliyekuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula. ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Makampuni ya Bravo, ambayo ni kampuni mama ya Bravo Logistics na Agricom Africa, akimtambulisha Group CEO wa Makampuni hayo, Alex Duffar, (kulia) kwa Makamu wa Rais, Dk. Philip Isidor Mpango (wa pili kushoto), wakati wa hafla ya siku ya Sekta Binafsi nchini, TPSF Day. Kushoto ni Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji kushoto nyuma ni na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki.

Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. (Kuna baadhi ya mambo, ili kupata mafanikio, lazima uajiri watu wenye uwezo na uzoefu wa kimataifa!, huyu Mama, Angelina Ngalula, amewaacha wabongo wote na kuajiri mzungu as Group CEO, sasa Kampuni ya Agricom ndio inayoongoza Tanzania kwa uuzaji wa ma trekta na zana za kilimo, huku tuna makampuni ya wazawa, kama Suma JKT yana sua sua!. Hivyo tukubali tukatae, ili ATC izalishe kwa faida, top lazima awe ni mwenye uzoefu wa ukweli na sio uzalendo. Hata SGR, we need more able people!

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hii, Pascal Mayalla, (ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, na wakili wa kujitegemea kwa kujitolea kutoa msaada wa kisheria), wakati wa hafla ya siku ya Sekta Binafsi nchini, TPSF Day. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Bravo Group, ambayo ni kampuni mama wa Agricom Africa, Bw. Alex Duffar, akionyesha cheti cha kupongezwa kuwa mmoja wa wadhamini wa siku ya Sekta Binafsi nchini, TPSF Day, iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Bravo Group, ambayo ni kampuni mama wa Agricom Africa, Bw. Alex Duffar, akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hii, Pascal Mayalla, (ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, na wakili wa kujitegemea kwa kujitolea kutoa msaada wa kisheria), wakati wa hafla ya siku ya Sekta Binafsi nchini, TPSF Day, iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Bravo Group, ambayo ni kampuni mama wa Agricom Africa, Bw. Alex Duffar, akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni siku ya Sekta Binafsi nchini, TPSF Day, iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Bravo Group, ambayo ni kampuni mama wa Agricom Africa, Bw. Alex Duffar, akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni siku ya Sekta Binafsi nchini, TPSF Day, iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Bravo Group, ambayo ni kampuni mama wa Agricom Africa, Bw. Alex Duffar, akizungumza siku ya Sekta Binafsi nchini, TPSF Day, iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.





Mtendaji Mkuu wa kundi la makampuni ya Bravo Group, ambayo ni kampuni mama wa Agricom Africa, Bw. Alex Duffar, kwenye picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Agricom Africa, siku ya Sekta Binafsi nchini, TPSF Day, iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad