SERIKALI YAKUBALI NA KUPOKEA HOJA YA CRASA KUHUSU KUPUNGUA KWA GHARAMA ZA MAWASILIANO NJE YA MPAKA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 21, 2022

SERIKALI YAKUBALI NA KUPOKEA HOJA YA CRASA KUHUSU KUPUNGUA KWA GHARAMA ZA MAWASILIANO NJE YA MPAKA

 Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Zanzibar Mhe. Dkt Khalid S. Mohamed (wa pili kushoto) akiondoka ukumbini muda mfupi baada ya kutekeleza zoezi la ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Uchumi ya Umoja wa Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano Kusini mwa Afrika (CRASA), ulioratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kufanyika unguja. Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Zanzibar Mhe. Dkt Khalid S. Mohamed (wa tatu kulia) muda mfupi kabla ya kutekeleza ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Uchumi ya Umoja wa Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano Kusini mwa Afrika (CRASA), ulioanza Jumatatu Novemba 21, 2022, Unguja. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Dkt Jabiri Bakari ambao ni wenyeji wa Mkutano huo, wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara na wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TCRA Mhandisi Othman Khatib.


Maafisa wa Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano za Tanzania na Zimbabwe wakifuatilia mada wakati wa Siku ya Kwanza na Mkutano na Semina kwa Kamati ya Uchumi (ERC) ya Chama cha Wadhibiti wa Mawasiliano Kusini mwa Afrika (CRASA), unaofanyika Unguja, Zanzibar chini ya uratibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhe. Dkt Khalid S. Mohamed.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TCRA Mhandisi Othman Sharif Khatib akifuatilia mwenendo wa matukio wakati wa ufunguzi wa Mkutano na Semina kwa Kamati ya Uchumi (ERC) ya Chama cha Wadhibiti wa Mawasiliano Kusini mwa Afrika (CRASA), unaofanyika Unguja, Zanzibar. Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Zanzibar Mhe. Dkt Khalid S. Mohamed.
Wawakilishi wa Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano za Madagascar na Malawi wakifuatilia mwenendo wa matukio wakati wa ufunguzi wa Mkutano na Semina kwa Kamati ya Uchumi (ERC) ya Chama cha Wadhibiti wa Mawasiliano Kusini mwa Afrika (CRASA), unaofanyika Unguja, Zanzibar. Kutoka kushoto ni Meneja wa Idara ya Masuala ya Uchumi ya Mamlaka ya Mawasiliano Malawi Bi. Linda Kambale, na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Madagascar Bw. Brillant Rakotoratsimanjefy.
Maafisa Waandamizi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Msumbiji (INCM) Bw. Lucio Cardoso (wa kwanza kushoto), Bw. Abdul Amid (katikati) na Oliveira Joaquim Zindoga (wa kwanza kulia), wakifuatilia mada wakati wa semina ya Mafunzo kuhusu bei za Mawasiliano na uchambuzi wa Taarifa za sekta ya Mawasiliano iliyowasilishwa na wawezeshaji (hawamo pichani) kutoka Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU). Semina hiyo ya siku nne imeandaliwa na Chama cha Wadhibiti wa Mawasiliano Kusini mwa Afrika (CRASA) kwa ushirikiano na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), na kufunguliwa Jumatano Novemba 21, 2022 na Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Zanzibar Mhe. Dkt Khalid S. Mohamed.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Dkt Jabiri Bakari akiwasilisha hotuba ya ukaribisho kwa wajumbe wa Mkutano wa Kamati ya Uchumi ya Umoja wa Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano Kusini mwa Afrika (CRASA), ulioanza Jumatatu Novemba 21, 2022, ukifanyika Unguja, Zanzibar; Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Zanzibar Mhe. Dkt Khalid S. Mohamed.
Ofisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw. Nelson Mwalongo (kulia) akimsajili Ofisa wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi-Zanzibar Mhandisi Issa Hamad Bakar, wakati wa siku ya kwanza ya Semina ya mafunzo ya uchambuzi wa taarifa za mawasiliano iliyoandaliwa na Kamati ya Uchumi ya Umoja wa Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano Kusini mwa Afrika (CRASA) na kufanyika Unguja, Zanzibar. Semina hiyo ilifunguliwa na Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi-Zanzibar Mhe. Dkt Khalid S. Mohamed.
Afisa Habari wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Bw. Kassim Salum Abdi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad