WAJASIRIAMALI TEMEKE WAASWA KURASIMISHA BIASHARA ZAO ILI KUWEZA KUPATA MIKOPO KUTOKA MANISPAA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 16, 2022

WAJASIRIAMALI TEMEKE WAASWA KURASIMISHA BIASHARA ZAO ILI KUWEZA KUPATA MIKOPO KUTOKA MANISPAA

 


Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Temeke, Diwani wa kata ya Sandali, Christofa Mwansasu akizungumza wakati wa kongamano la Vijana lililofanyika katika manispaa ya Tekeme na Kuandali wa Akili ya Pesa Challenge Julai 15,2022 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Vijana walio shiriki katika Akili ya Pesa Callenge wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

WAJASIRIAMALI wadogo wadogo wa manispaa ya Temeke wameaswa kurasimisha biashara zao za ujasiliamali ili waweze kufikiwa na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali kupitia mfuko wa Vijana katika manispaa hiyo

Hayo yamesemwa na Mwanzilishi wa Akili ya Pesa Challenge, Maida Waziri, wakati akizungumza kwenye wa kongamano la vijana wajasiriamali wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Julai 15, 2022. lililoandaliwa na Akili ya Pesa Challenge, amesema kuwa Wajasiriamali hao wa Temeke wanafanya biashara mbalimbali kama Mama ntilie, wauzaji wa mitumba, wasafirishaji, wachimbaji wa visima na wasanii.

Amesema zote hizo ni biashara kama zikirasimishwa kwenye mamlaka husika zitawawezesha kupata mikopo mbalimbali inayotolewa na Manispaa hiyo isiyo na riba kwa vijana.

"Nawahamasisha vijana kuhusu ujasiriamali lakini pia muweze kujua fursa zilizozunguka kwa wilaya ya Temeke, ukiangalia Tekeme kuna Viwanja vya Mpira kama Uwanja wa Benjamini Mkapa, Uwanja wa Uhuru, uwanja wa Azam.

Lakini ukiangalia kunamasoko makubwa ya Mboga mboga, Mchele, haya yoto yapo wilaya ya Temeke, Reli ya Tazara imepakana na Temeke, Uwanja wa Ndege umepakana na Tekeme zote hizi ni fursa." Amesema Maida

Amesema kuwa Manispaa ya Temeke yenyewe inafursa nyingi zinazotakiwa kwenda kwa vijana.

"Sisi kama Akili ya Pesa Challenge tumeona Changamoto ya vijana wengi wanapewa fedha za mikopo wanashindwa kufanya biashara pia wanapewa mikopo wanashindwa Kurudisha pamoja na mikopo hiyo kutokuwa na riba, tumeona tuweke shindano hili leo kuwashindanisha ili washindi washindanie shilingi Milioni sita, ikiwa mshindi wa kwanza atapata milioni tatu, wapili milioni mbili na watatu apate milioni moja.

"Vigezo tunavyovichukua kwenye Akili ya Pesa Challenge ni mjasiliamali ambaye umeshaanza kufanya biashara na sio ambao wanasubiri washinde ndio waanze biashara." Amesema Maida

Maida amesema sio kuwapa fedha bali kuibua na kuleta chachu kwa vijana wajue hakuna njia pekee inayoweza kuwapa mafanikio zaidi ya kujiajiri na kuajiri wengine.

Amesema kuwa katika kongamano hilo Vijana wanaonana na watu wanaofanya vizuri katika sekta mbalimbali kama wafanyabiashara wakubwa, vijana wenzao ambao wamefanikiwa katika sekta mbalimbali.

"Kwenye Akili ya pesa tunatoa elimu ya ujasiliamali kwa vijana. Waliokuja hapa wote ni wajasiliamali wameshaanza ujasiliamali."

Kwa Upande wa Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Temeke, Diwani wa kata ya Sandali, Christofa Mwansasu amewapongeza Akili ya Pesa Challenge kwa kufanya Kongamano hilo Manispaa ya Temeke.

Amewaasa vijana kuchangamkia fursa zilizopo katika Manispaa hiyo ili waweze kujikwamua na changamoto mbalimbali za kimaisha.

Amesema watu wanaohamasisha vijana kujikwamua kiuchumi ni watu mhimu sana. Vijana wanapaswa kuwatumia na wasikae nao mbali kwa sababu mawazo yao yana tija, mawazo yao yanaonesha namna kutoka kwenye maisha kutoka hatua moja kwenda nyingine.

Amewatia moyo wadau wanaohamasiha vijana kujikwamua kiuchumia kwamba waendelee kuibua vipaji, kujuza ajira za vijana, waendelee kuonesha namna gani vijana wanaweza kunufaika ili tuweze kuondoa kizazi tegemezi kwa familia na jamii.

Kwa Upande wa Mjasiliamali wa kutengeneza Mikanda ya Gypusum, Hisham Mohamed Ally ameomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupunguza kodi kwa wajasiliamali wadogo wadogo.

Mjasiliamali wa Kuuza Korosho, Rahmat Issa amesema kuwa changamoto anayokutana nayo katika biashara yake ni mtaji na urasimishaji wa biashara.

Mnufaika wa Akili ya Pesa Challenge amewaasa vijana kutokukata tamaa kwenye biashara wanazozifanya.

Upande wa Mkazi wa Kata ya Sandari, Upendo Rashid kitu kilichomsukumba kushindania katika Akili ya Pesa Challenge ni kutaka kuonesha mfano vijana kutoka katika mtaa wa Sandali kwa sababu wengi walikuwa hawaamini na wengi walijua kuwa ni utapeli.

Amese kuwa kushirikia katika Akili ya Pesa Challenge kunamambo matatu ambayo ni kushinda, kushindwa na kujifunza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad