HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 14, 2022

ROYAL TOUR YAONGEZA WATALII IKOLOJIA

 Sehemu ya washiriki wa Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutembelea Hifadhi ya msitu wa Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi uliopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

 

Na Mwandishi Wetu

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania umesema tangu ilipozinduliwa filamu ya Royal Tour na Rais Samia Samia Suluhu Hassan idadi ya watalii wanaotembelea utalii Ikolojia imeongezeka kutoka watalii 49,000 kwa mwaka  hadi kufikia 150,000.

Umesema kutokana na kuongezeka kwa Wakala huo nao umeamua kuweka mikakati ya kuendelea kuboresha miundombinu ya hifadhi hizo ikiwemo kuboresha njia za kupita watalii,maeneo la malazi pamoja na kuwepo kwa maeneo mazuri ya kupumzikia.

Hayo yameelezwa leo Julai na Mkuu wa Kitengo cha Uhamasishaji Utalii katika Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Anna Lauwo wakati washiriki wa Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa  walipotembelea Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Samia kutangaza sekta ya utalii kupitia filamu ya Royal Tour pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani.

"Filamu ya Royal Tour imeongeza watalii kwa kiasi kikubwa na TFS imeongeza watalii wengi wa ndani pamoja na nje ,kwa mfano mwaka jana kabla ya Royal Tour idadi ya watalii ilikuwa inaanza 49000 lakini baada ya hii Royal Tour tumepata watalii 150,000.

"Ongezeko ni kubwa sana na katika kipindi kifupi, kwa hiyo unaona hii Royal Tour imehamasisha wengi kufahamu kumbe kuna utalii, kumbe Tanzania kuna kitu cha pekee ambacho sehemu nyingine hakipo na watu wameamka kumbe kuna umuhimu wa kwenda kupumzika , " Lauwo.

Kutokana na ongezeko hilo Lauwo amesema TFS wamejipanga vizuri kabisa akitoa mfano katika misitu yao yote nchini ukiwemo Pugu wameboresha miundombinu kama njia za kuingilia msituni ,wameboresha ya maegesho ya magari, wameboresha malazi kwa kujenga maeneo ya malazi na kuboresha yale yaliyopo kwa ajili ya kukidhi mahitaji.Aidha wanahamasisha  wawekezaji wa ndani na nje kuja kuwekeza kwenye huduma za malazi na chakula hasa loji ambazo haziharibu mazingira na makambi.

Kuhusu Msitu wa Pugu amesema msitu huo uko wilayani Kisarawe Kanda ya Mashariki na ni msitu ni moja kati ya Misitu 23 inayosimamiwa na  TFS ambayo imepandishwa hadhi kutoka Misitu ya asili na kuwa msitu wa Mazingira asilia kutokana na uwepo wa viumbe na mimea adimu ndani ya Misitu hiyo ambavyo havupatikani maeneo mengine ulimwenguni.

Amefafanua katika misitu hiyo 23 kuna vivutio vya aina mbalimbali ikiwemo maporomoko ya maji ambayo ni ya pili kwa urefu katika Bara la Afrika  yenye urefu wa mita 235 yanayopatikana hifadhi ya Kalambo.

Pia amesema kuna utalii mwingine unaofanyika kwenye mashamba ya miti yanayosamiwa na TFS akitokea mfano utalii wa kuendesha baiskeli, mazuri kwa mbio za  farasi na kutembea kwa miguu msituni.

"Kwa hiyo kwenye mashamba hayo Kuna maporomoko kwa mfano Meru Usa kuna maporokoko ya maji yenye urefu wa mita 70 lakini hayo watu hawayajui  wakati yapo  karibu kabisa na Mji wa Arusha ,ni sehemu nzuri ambayo watu wanaweza kwenda kutembea na kurudi.

"Katika hii misitu  yetu tunayofanya utalii Ikilojia haturuhusu kufanya shughuli nyingine yoyote isipokuwa utalii Ikilojia,utafiti pamoja na mafunzo na ndani ya hii Misitu tunahimiza sana uhifadhi wa mazingira kwasababu ndio kivutio kikubwa na hakuna kuangusha aina yoyote ya takataka wala kuchukua mdudu au mmea wa aina yoyote.

Akielezea zaidi amesema utalii Ikilojia ni zao jipya la utalii nchini ambalo halijulikani na wengi lakini linamanufaa makubwa katika ya binadamu kwasababu ni maeneo tulivu na yenye hewa safi na ndio sehemu pekee unayoweza kupumzika na kuondoa msongo wa mawazo.

Pamoja na hayo Lauwo  wamewahimiza Watanzania watembelee msitu wa Hifadhi ya mazingira Pugu Kazimzumbwi ambao uko karibu kabisa na Dar es Salaam, unaweza kwenda na kurudi lakini ukitaka kulala yako maeneo  ya malazi.

Akielezea faida za Msitu wa Pugu mbali ya utalii amesema  kuna  hewa safi kabisa ambayo Dar es Salaam huwezi kuipata."Msitu  huu tunasema ni mapafu ya Dar es Salaam,na tunafahamu kwa  sasa hivi tunasema hali ya hewa imebadlika sana

"Na saa zingine hewa inakuwa joto au baridi sana.Hayo yote ni mabadiliko ya tabianchi lakini kuifanya hewa irudi kama awali tunahimiza uhifadhi wa misitu.Kwasababu  Msitu wenyewe kama ulivyo unavuta hewa chafu na kutoa hewa safi ndio maana tunaita mapafu ya Dar es Salaam."

Kuhusu viingilio amesema mtu mzima ni Sh.2000 lakini wenye umri wa miaka Sita hadi miaka 17 ni Sh.1000 na walio na umri kuanzia miaka mitano kushuka chini ni bure.







 


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad